Pata taarifa kuu

Mali: Marekani inataka hatua ya kuondoka kwa UN kufanyika kwa mpangilio

NAIROBI – Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imetoa wito wa kufutwa kwa "utaratibu na kuwajibika" kwa tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Mali, Minusma, kufuatia wito wa Bamako wa kutaka ujumbe huo kuondoka bila “kuchelewa".

Utawala wa kijeshi wa Mali umetoa wito kwa walinda usalama wa UN kuondoka bila kuchelewa
Utawala wa kijeshi wa Mali umetoa wito kwa walinda usalama wa UN kuondoka bila kuchelewa AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Tuna wasiwasi kuhusu athari zitakazotokana na hatua hii haswa katika hali suala la kiusalama na hali ya kibinadamu masuala yanayowakabili wakazi wa Mali. Tutaendelea kushirikiana na washirika wetu katika eneo la Afrika Magharibi kuwasaidia kukabiliana na changamoto za dharura za kiusalama na matatizo ya kiutawala yanayowakabili," Marekani ilisema.

"Tunakaribisha mashauriano zaidi na viongozi wa kanda kuhusu hatua za ziada za kuendeleza hali ya utulivu na kuzuia migogoro."

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliongeza kuwa serikali ya Mali inayoongozwa na jeshi "lazima ifuate ahadi zake zote", haswa katika suala la kurejeshwa kwa utawala kiraia ifikapo Machi 2024.

Mali inamtuhumu Minusma, ambayo mamlaka yake ya sasa yanaisha wiki ijayo, kwa "kushindwa" kukabiliana na  changamoto za usalama.

Waziri wa Mambo ya nje wa Mali Ijuma ya wiki iliyopita mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alitaka walinda usalama hao "kuondoka bila kuchelewa" nchini mwake (MINUSMA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.