Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Sudan: 'Vurugu zinaendelea' Darfur yaonya MSF, wakimbizi wanamiminika Adré, Chad

Mashambulio ya anga, milio ya risasi na milipuko ya mabomu yatikisa Khartoum Jumamosi hii, huku ghasia huko Darfur (magharibi) zikiendelea kusababisha wakaazi kutoroka. Mapigano yalianza tena siku chache zilizopita huko Darfur, hasa huko El Geneina, na katika maeneo mengine kadhaa karibu na mpaka wa Chad. Mapigano mapya yanasababisha wakaaji wa jiji hili kukimbilia Chad, Adré, au karibu na mpaka wa upande wa Sudan.

Sudan: Hospitali ya El-Geneina, Darfur Magharibi, Mei 2023.
Sudan: Hospitali ya El-Geneina, Darfur Magharibi, Mei 2023. ABBAS HUSSEIN ALTOM via REUTERS - ABBAS HUSSEIN ALTOM
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi hii, mashambulizi ya anga yamelenga eneo la Yarmouk kusini mwa mji mkuu, na kusababisha "waathiriwa wa kiraia", kulingana na kamati ya upinzani ya eneo hilo, moja ya makundi ya wanamgambo ambayo hupanga misaada ya pande zote kati ya wakaazi wa mji mkuu. Risasi kutoka vyanzo mbalimbali pia zimeripotiwa na wakazi wa kusini mwa Khartoum, huku katika vitongoji vya kaskazini kukisikika "milio ya roketi na mizinga mikubwa", walioshuhudia wameliambia shirika la habari la AFP.

Hali inatisha vile vile katika eneo la Darfur, ambako "vurugu zinaendelea", linaonya shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF). Ushuhuda wa unyanyasaji mkubwa dhidi ya raia unaongezeka, na kulingana na UN, zaidi ya watu 149,000 wamekimbilia Chad tangu mapigano yalipoanza. Katika siku za hivi karibuni pekee, "watu 6,000 wameukimbia mji wa El-Geneina" (Darfur Magharibi), kupata hifadhi katika mji wa Adré nchini Chad, MSF imesema leo Jumamosi.

Kati yao, zaidi ya 400 walijeruhiwa, 120 kati yao wako katika hali mbaya. Houda Ibrahim, kutoka timu ya wahariri ya Afrika, amemhoji Claire Nicolet, mkuu wa shughuli za Sudan na mashariki mwa Chad katika shirika la Madaktari Wasio na MipakaMédecins sans frontières.

"Huko Adré, tulipokea zaidi ya majeruhi 400, wengi wao wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi kufuatia mapigano makali sana huko Geneina, au hata kujeruhiwa barabarani tukimwacha Geneina kuelekea Adré. Kwa hivyo leo tuko katika hospitali ya Adré, tunashughulikia kesi hizi na wagonjwa zaidi ya 200 ambao wanapaswa kuingia kwenye chumba cha upasuaji. Pia tunaona zaidi ya wakimbizi 15,000 ambao wameondoka Geneina katika siku za hivi karibuni, hali ambayo ina maana kwamba wakazi hatimaye wanafanikiwa kuondoka Geneina, ambapo kwa miezi miwili barabara hii imekuwa ikitumika kwa shida na hatujapokea wagonjwa moja kwa moja kutoka Geneina.

Miezi miwili ya vita nchini Sudan imesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la ACLED. Zaidi ya watu milioni 2.2 wameikimbia nchi hiyo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, huku wakimbizi 528,000 wamepata hifadhi katika nchi jirani. Licha ya majaribio ya upatanishi yaliyoongozwa hasa na Riyadh na Washington, hakuna hali ya kurejea kwa amani inayoonekana.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.