Pata taarifa kuu

Zimbabwe: Wanaharakati 39 wa upinzani wafunguliwa mashtaka

NAIROBI – Mamlaka nchini Zimbabwe zimewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani baada ya ofisi ya chama tawala ZANU-PF kuharibiwa, jumatatu kuelekea uchaguzi wa mwezi Agosti.

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa, mpizani wa rais Emmerson Mnangagwa
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa, mpizani wa rais Emmerson Mnangagwa REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Mashatka dhidi ya 39 hao yanajiri wakati huu taharuki ya kisiasa ikiendelea kupanda nchini Zimbabwe, uchaguzi ukitarajiwa mwezi agosti.

Waendesha mashtaka wamesema washukiwa waliharibu nyumba kadhaa eneo la Nyatsime na hilo limesabisha uharibu mkubwa kwa wenyeji, mashtaka ambayo washtakiwa wanadai yanachochewa kisiasa.

Washtakiwa ni wafuasi wa chama cha Citizens Coalition for Change chake Nelson Chamisa mpizani mkuu wa rais Emmerson Mnangagwa kwenye uchaguzi ujao.

Ni mashtaka yanayojiri wakati huu upinzani na mashirika ya kiraia yakilalamikia hatua ya serikali kujaribu kuwanyamazisha kuelekea uchaguzi mkuu.

Chama twala nchini Zimbabwe kimekuwa madarakani tangu mwaka 1980.

Wakosoaji wameishutumu serikali kwa kutumia mahakama kuwalenga wanasiasa wa upinzani na kusema kumekuwa na ongezeko la ukamataji kiholela na ukandamizaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.