Pata taarifa kuu

Sudan: Mashambulio ya anga yaripotiwa kwenye baadhi ya maeneo mjini Khartoum

NAIROBI – Mashambulio ya anga, roketi na risasi yameripotiwa katika maeneo kadhaa ya jiji la Khartoum hapo jana, wakati huu mapigano kati ya pande zinazohasimiana yakiingia siku ya tatu tangu kumalizika kwa muda was aa 24 wa kusitisha mapigano, maelfu ya raia wakinaswa kwenye vita.

Mapigano yameripotiwa katika baadhi ya maeneo mjini Khartoum wakati huu wito ukitolewa wa kusitishwa kwa vita
Mapigano yameripotiwa katika baadhi ya maeneo mjini Khartoum wakati huu wito ukitolewa wa kusitishwa kwa vita REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Ni mapigano ambayo sasa mashirika ya misaada yanasema yamesababisha maelfu ya raia walioko mjini Khartoum na miji jirani, kushindwa kutoka nje ambapo pia yametatiza shughuli za utoaji wa misaada kwa raia wanaohitaji.

Vita kati ya jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, sasa imeingia karibu mwezi wa pili, ambapo imesababisha watu karibu milioni 2 kukimbia nchi yao huku uchumi wa taifa hilo ikiendelea kuporomoka na mamia ya raia wakikosa maji na umeme.

Licha ya majadiliano yanayoongozwa na Saudi Arabia na Marekani mjini Jeddah, wapatanishi wameshindwa kuzishwaishi pande zinazohasimiana kusitisha mapigano, huku mzozo ukishika kasi kuansia siku ya Jumapili saa chache baada ya mudaa wa saa 24 kumalizika.

Wakati huu wapiganaji wa RSF wakifanikiwa kuchukua maeneo mengi ya mji wa Khartoum na hata kuweka kambi katika makazi ya raia, jeshi la Serikali limeendelea kubaki na faida ya ndege za kivita ambazo zimekuwa zikishambulia kutokea angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.