Pata taarifa kuu

Watoto 300 wahamishwa kutoka kituo cha watoto yatima Khartoum

Wakiwa wamenaswa na vita nchini Sudan, watoto 300, "wengine wakiwa wamedhoofika sana" kwa kukosa chakula, walihamishwa siku ya Jumatano kutoka kwenye kituo cha watoto yatima huko Khartoum baada ya vifo vya wakaazi wengine, vyanzo vya kibinadamu viliiambia AFP siku ya Alhamisi.

Watoto kutoka katika kituo hiki cha watoto yatima walifariki baada ya kuugua "homa, upungufu wa maji mwilini, magonjwa na utapiamlo", kulingana na UNICEF.
Watoto kutoka katika kituo hiki cha watoto yatima walifariki baada ya kuugua "homa, upungufu wa maji mwilini, magonjwa na utapiamlo", kulingana na UNICEF. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha watoto yatima ambacho kinapatikana katikati mwa mji mkuu wa Sudan, kiko katika kitongoji kilichoathiriwa sana na mapigano ambayo yamehusisha jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane dhidi ya wanamgambo wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo tangu Aprili 15.

"Watoto mia tatu na wafanyakazi 70 wa kituo cha watoto yatima cha Maygoma" walihamishwa kwenda mji wa Madani, kilomita 200 kusini mwa Khartoum, Alyona Synenko, msemaji wa shirikisho la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) ameliambia shirika la habari la AFP. "Tulmengilia kati kufuatia ombi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii ambalo kituo hiki cha watoto yatima kiko chini ya mamlaka yake," ameongeza.

Katika wiki za hivi karibuni, watoto kutoka kituo hiki cha watoto yatima walifariki dunia baada ya kuugua "homa, upungufu wa maji mwilini, ugonjwa na utapiamlo", afisa wa mawasiliano wa UNICEF katika eneo hilo Ammar Ammar ameliambia shirika la habari la AFP. "Ilikuwa ni lazima kupata, kutoka kwa pande zinazozozana, dhamana muhimu ili kuhakikisha njia salama ya watoto na wafanyakazi wa kituo cha watoto yatima," ameongeza Bi. Synenko.

"Wana umri kati ya mwezi mmoja na miaka 15", watoto "wameishi katika nyakati ngumu sana", almesema Jean-Christophe Sandoz, mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Sudan, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Alhamisi na shirika hilo. "Tunazungumza kuhusu watoto wanaohitaji uangalizi maalum wa kimatibabu ambao wamekosa chakula kwa wiki kadhaa: hii ndiyo ilifanya upasuaji kuwa mgumu sana, baadhi yao wakiwa dhaifu sana", amebainisha Bi Synenko.

Baada ya kufika Madani, watoto hao waliwekwa chini ya ulinzi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii. Hospitali zilizo katika maeneo ya mapigano hazifanyi kazi tena, wakati hazijafungwa. Na mgogoro unapaswa kuwa mbaya zaidi kutokana na kukaribia kwa msimu wa mvua, sawa na kuzuka upya kwa malaria, uhaba wa chakula na utapiamlo wa watoto.

Kwa mujibu wa UNICEF, zaidi ya watoto milioni 13.6 wanahitaji misaada ya kibinadamu ili kuishi nchini Sudan. Miongoni mwao, 620,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali, ambao nusu yao wanaweza kufa ikiwa hawatasaidiwa kwa wakati, linaonya shirika hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.