Pata taarifa kuu

Viongozi wa Afrika wanasema wako tayari kwa upatanishi nchini Urusi na Ukraine

Viongozi wa Afrika, wanaotaka kusaidia kumaliza vita, walikubaliana Jumatatu kwa ujumbe wa upatanishi katikati ya mwezi Juni kati ya Urusi na Ukraine, ofisi ya rais wa Afrika Kusini imetangaza Jumanne.

"Dhamira yetu ni dhamira ya amani, na tunataka kuiita njia ya amani," aliongeza rais wa Afrika Kusini
"Dhamira yetu ni dhamira ya amani, na tunataka kuiita njia ya amani," aliongeza rais wa Afrika Kusini REUTERS - ESA ALEXANDER
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alionyesha kuwa viongozi wenzake wa Urusi na Ukraine, Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky, wametoa makubaliano yao ya kupokea ujumbe huu wa amani unaojumuisha viongozi sita wa Afrika. Wawakilishi hao walikutana karibu Jumatatu na "kukubali kupendekeza vipengele" kwa Urusi na Ukraine "kwa ajili ya kusitishwa kwa mapigano na amani ya kudumu ipatikae katika eneo hilo", imesema taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa huduma za Rais wa Afrika Kusini.

"Wakuu wa nchi (kutoka Afrika) wamethibitisha kuwa na muda wa kwenda Ukraine na Urusi katikati ya mwezi Juni," taarifa hiyo imeongeza bila kutoa tarehe maalum. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi sita zinazohusika "watakamilisha vipengele vya ramani ya kuelekea amani", imesema taarifa hiyo.

Mkutano wa Jumatatu "ulithibitisha kwamba sasa tuko katika hatua ambayo tutaenda Kyiv na Moscow," Ramaphosa alisema baadaye wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenzake wa Ureno, Marcelo Rebelo de Sousa. "Dhamira yetu ni dhamira ya amani, na tunataka kuiita njia ya amani," alisema Afrika Kusini, akiongeza kwamba viongozi wa Afrika "watajaribu kupata ahadi kutoka kwa pande zote mbili ambazo wao pia wanapaswa kutafuta (...) kumaliza mzozo huu kwa njia za amani".

'Kima cha chini cha mahitaji'

Viongozi wa Urusi na Ukraine "lazima watufafanulie maoni yao kuhusu vita na vile vile mahitaji yao ya chini ili kumaliza mzozo", pia alisema. "Tutaweza kutoa maoni yetu kama Waafrika juu ya jinsi tunavyoona athari za vita hivi kwa Afrika katika bei ya chakula, nafaka na bei ya mafuta, na pia kwa Ulaya na ulimwengu wote kwa sababu ya kuwa aina ya migogoro ya kimataifa," Ramaphosa alisema.

Marcelo Rebelo de Sousa, ambaye alimshukuru Bw. Ramaphosa kwa jukumu lake katika mpango huo, kwa upande wake alisisitiza umuhimu wa kusikiliza "pande zote mbili na kuwaambia nini maono ya Afrika kwa vita ambavyo sio tu vita vya Ulaya, ni vita vya utandawazi”.

Wajumbe wa ujumbe huo, waliotambuliwa mwezi uliopita na rais wa Afrika Kusini, ni pamoja na viongozi wengine wa Congo-Brazzaville, Misri, Senegal, Uganda na Zambia. Mkuu wa Nchi ya Comoro, Azali Assoumani, alihudhuria mkutano wa Jumatatu katika nafasi yake kama mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.

Afrika inakabiliwa na ongezeko la bei ya nafaka na matokeo ya vita kati ya Urusi na Ukraine katika biashara ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.