Pata taarifa kuu

Sudan: Watu 180 wamezikwa bila ya kutambuliwa: Shirika la msalaba mwekundu

NAIROBI – Nchini Sudan, watu 180 wamezikwa bila ya kutambuliwa, kwa mujibu wa maafisa wa Shirika la msalaba mwekundu, kutokana na mapigano yanayoendelea jijini Khartoum na Darfur. 

Mapigano yanaendelea nchini Sudan licha ya juhudi za upatanishi
Mapigano yanaendelea nchini Sudan licha ya juhudi za upatanishi AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema tangu mapigano hayo yalipoanza zaidi ya mwezi mmoja ulopita, miili ya watu 102 imezikwa katika makaburi ya  Al-Shegilab jijini Khartoum, huku wengine 78 wakizikwa katika makaburi ya Darfur. 

Maafisa hao wanasema, ilikuwa ni vigumu kwenda mitaani na kuwatambua watu waliopoteza maisha, kwa sababu ya utovu wa usalama. 

Mauaji hayo yalitokea licha ya pande hizo mbili kuelewana kusitisha vita ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia watu waliothiriwa na mapigano hayo. 

Watu zaidi ya 1800 wameauawa kwenye mzozo huu wakati huu mazungumzo kati ya  Jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Saudi Arabia yakikwama. 

Katika hatua nyingine, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeongeza muda wa ujumbe wake wa kisiasa nchini Sudan ukiongozwa na mjumbe wake Volker Perthes kwa miezi sita zaidi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.