Pata taarifa kuu
SHERIA-HAKI

DRC: Mbunge Edouard Mwangachuchu akabiliwa na kifungo cha maisha

Mbunge wa kitaifa Édouard Mwangachuchu kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini amefikishwa tena mahakama, baada ya kukamatwa na kuwekwa siku chache, katika gereza la kijeshi la Ndolo mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Maficho mawili ya silaha za vita yaligunduliwa katika shamba yake huko Masisi katika mkoa wa Kivu Kaskazini na pia katika makazi yake huko Kinshasa, mnamo mwezi wa Februari.

Gereza la kijeshi la Ndolo, mjini Kinshasa, Februari 15, 2023.
Gereza la kijeshi la Ndolo, mjini Kinshasa, Februari 15, 2023. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Kamanda wa Kamanda-Muzembe

Édouard Mwangachuchu ambaye alikamatwa tangu Machi 1 na kushtakiwa kwa ujasusi na M23, anakabiliwa na kifungo cha maisha. Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 70, anaonekana kuwa mgonjwa sana. Mawakili wake wanaendelea kuomba aachiliwe kwa masharti kwa sababu za kiafya. Uukubwa wa mashitaka unaweza kutatiza mchakato huu.

Édouard Mwangachuchu amedhofika kimwili, almeonekana akitembea kwa msaada wa mkongojo, kwa sababu ilikuwa vigumu kusimama kwa muda mrefu. Anadai kuwa na maumivu ya moyo. Akishtakiwa kwa madai ya vitendo vya kushiriki katika harakati za uasi, ujasusi na kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria, mbunge huyu wa kitaifa kutoka Masisi anakanusha mashtaka yote dhidi yake.

Akionyesha waraka, mtu huyo anasema aliidhinishwa kushika silaha ya vita na risasi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Muyej Manez, chini ya utawala wa Joseph Kabila. Hata hivyo, mwendesha mashitaka anahoji uhalisia wa hati iliyoonyeshwa na mshtakiwa Mwangachuchu. Kwa upande wa wanasheria wa serikali, ni Rais wa Jamhuri pekee ndiye mwenye uwezo wa kutoa, kwa amri, idhini hii ya kumiliki silaha, kwa mujibu wa masharti ya sheria. Hivyo kuna haja ya kumfikisha mahakamani aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Muyej Manez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.