Pata taarifa kuu
HAKI-ULINZI

Waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Burkina Faso Zida yafutwa

Mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou imefuta waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Burkina Faso Yacouba Isaac Zida kulingana na shirika la habari la AFPlikimnukuu wakili wake na chama chake, na kuandaa njia ya uwezekano wa kurejea nchini Burkina Faso baada ya miaka saba akiwa uhamishoni nchini Canada.

Yacouba Isaac Zida, wakati huo luteni-Colonel, alichukua mamlaka mnamo Novemba 1, 2014, siku moja baada ya Blaise Compaoré kutimuliwa madarakani kufuatia maandamano ya kiraia.
Yacouba Isaac Zida, wakati huo luteni-Colonel, alichukua mamlaka mnamo Novemba 1, 2014, siku moja baada ya Blaise Compaoré kutimuliwa madarakani kufuatia maandamano ya kiraia. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, "mahakama ya kijeshi ilitangaza kuwa haina uwezo wa kutoa uamuzi juu ya kesi ambayo Bw. Zida anashitakiwa kwa makosa ya 'utoro wakati wa amani' na 'kukataa kutii'", mmoja wa wanasheria wake, Me Salifou Dembélé, ameliambia shirika la habari la AFP. Jaji wa kijeshi pia ameagiza kuondolewa kwa "waranti wa kimataifa wa kukamatwa" dhidi yake, ameongeza.

Ni kwa furaha na shangwe chama cha UNIR-MPS kimepokea uamuzi huo", chama cha Bw. Zida kimeandika. "Chama cha UNIR-MPS kinakaribisha ujasiri, ukomavu na uhuru wa mahakama yetu ya kijeshi, ambayo imeweza kujinasua bila ushawishi wowote kwa kutoa uamuzi sahihi, na hakuna chochote isipokuwa sheria, kwa uwajibikaji kamili", inaendelea taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na naibu kiongozi wa chama, Athanase Boudo.

Chama kinataka "kufanya maandalizi ya kurejea, kwa wakati ufaao, kwa mwenzetu ambaye kila mara ameeleza nia yake ya kuchangia katika mapambano ambayo raia wa Burkina Faso wanafanya dhidi ya ugaidi".

Yacouba Isaac Zida, ambaye wakati huo alikuwa luteni kanali, alichukua mamlaka mnamo Novemba 1, 2014, siku moja baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré, aliyetimuliwa madarakani maandamano ya kiraia baada ya miaka 27 madarakani.

Baada ya shinikizo kali kutoka kwa vyama vya siasa, mashirika ya kiraia na jumuiya ya kimataifa, aliachia madaraka baada ya wiki tatu kwa Michel Kafando, mwanadiplomasia mstaafu ambaye alimteua mara moja kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya mpito.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito (mwezi Desemba 2015), Bw. Zida alijiunga na familia yake nchini Canada Januari 2016 kwa ruhusa iliyotolewa na Rais Roch Marc Christian Kaboré. Likizo yake iliisha baada ya Februari 15, 2016 na Bw. Kaboré akamwamuru arejee katika kambi yake, bila mafanikio. Muda mfupi baadaye, aliachizwa kazi ya jeshi na rais wa kijeshi kwa "kutoroka jeshi wakati wa amani" na "kutotii".

Mnamo mwezi Septemba 2016, kesi za kijeshi za "utoro wakati wa amani" dhidi ya Bw. Zida ziliamriwa na Rais Kaboré. Yacouba Isaac Zida, ambaye kurejea kwake kumetangazwa mara kadhaa na ndugu zake na washirika wake wa karibu bila hata hivyo kutekelezwa, alikuwa mgombea wa uchaguzi wa urais wa 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.