Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Wananmgambo wa Kiislam wamgeukia mshirika wao muhimu, Burhane

Jenerali Abdel Fattah al-Burhane amekuwa vitani kwa muda wa wiki sita dhidi ya makamu wake wa zamani Mohamed Hamdane Daglo nchini Sudan, lakini vita vya pili vimefunguliwa dhidi yake: wanamgambo wa Kiislam walioazimia kumalizana na afisa wanayemchukulia kuwa anapatana sana na adui.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, Oktoba 2021 mjini Khartoum.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, Oktoba 2021 mjini Khartoum. © Ashraf Shazly/AFP
Matangazo ya kibiashara

Chini ya udikteta wa Jenerali Omar al-Bashir, ambaye aliingia madarakani kwa mapinduz ya kijeshi mwaka 1989, wanamgambo wa Kiislamu walichangia kwa mapinduzi hayo. Walianzisha mtandao mkubwa wa kifedha, kibiashara na kisiasa.

Katika miaka 67 ya uhuru, Sudan imetumia zaidi ya miaka 55 chini ya ushawishi wa majenerali, inakumbuka Taasisi ya Rift Valley. "Kwa hivyo siasa za Sudan asili yake ni za kijeshi na jeshi ni taasisi iliyo na siasa," kituo cha utafiti kinaendelea.

Mnamo mwaka wa 2019, wakati jeshi lililazimika kumuondoa Bashir kwa shinikizo kutoka mitaani, wanamgambo wa Kiislamu walilazimika kujiuzulu na kufuatilia siasa chini kwa chini. Chama cha National Congress cha Bashir kilipigwa marufuku na maafisa kadhaa wa zamani wa udikteta walifungwa gerezani. Na jeshi, likiwa na hamu ya kutuliza maandamano ya raia na jumuiya ya kimataifa, lilichagua "afisa asiyejulikana" - Jenerali Burhane - kuchukua uongozi wa nchi, amesema mtafiti Alex de Waal.

Jenerali Burhane kisha alianza kuzidisha matamko ya chuki dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu na maafisa wakuu wa zamani wa utawala wa Bashir, hasa dhidi ya chama cha National Congress. Lakini ikiwa Burhane alitoa ahadi kwa jumuiya ya kimataifa kwa kujitenga na utawala wa zamani, wanamgambo wa Kiislamu walimkumbuka wakati vita vilipozuka Aprili 15: Chama cha National Congress kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuelezea uungaji mkono wake kwa jeshi, ambalo anaongoza.

Wanamgambo wa Kiislamu "wanatumia mazingira ya kipekee ili kuhakikisha nafasi yao katika nyanja ya kisiasa ya siku zijazo", Othmane al-Mirghani, mkuu wa Gazeti huru la kila siku la al-Tayar ameliambia shirika la habari la AFP.  Hivi karibuni Jenerali Burhane alituma barua kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuomba kubadilishwa kwa mjumbe wake nchini Sudan, Volker Perthes.

Vituo vya televisheni vya Kiislamu na vinavyomuunga mkono Bashir - vyote vikiwa ng'ambo - sasa vinamtuhumu Jenerali Burhane mara kwa mara kuwa amekuwa nguzo ya wanamgambo na Daglo, lakini pia kwa kuwapa silaha na ufadhili. "Yeye ni mwanajeshi: misheni yake inaisha kwa kila kampeni," amesema Bw. Mirghani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.