Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Shambulio jipya dhidi ya walinzi wa mbuga ya Virunga laua wawili

Walinzi wawili wa mazingira wameuawa siku ya Jumapili katika shambulio jipya kwenye Mbuga ya Kitaifa ya Virunga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamlaka ya usimamizi wa mbuga hiyo imesema.

DRC: Mazishi ya mmoja wa walinzi wa mbuga ya kitaifa ya Virunga, aliyeuawa katika shambulio la Jumapili Januari 10 asubuhi. Walinzi sita wa mbuga hii waliuawa na mwingine kujeruhiwa na wavamizi waliokuwa na silaha kulingana na huduma ya mawasiliano ya hifadhi hiyo.
DRC: Mazishi ya mmoja wa walinzi wa mbuga ya kitaifa ya Virunga, aliyeuawa katika shambulio la Jumapili Januari 10 asubuhi. Walinzi sita wa mbuga hii waliuawa na mwingine kujeruhiwa na wavamizi waliokuwa na silaha kulingana na huduma ya mawasiliano ya hifadhi hiyo. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili, mamlaka ya mbuga hiyo imesema washambuliaji hao wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la "Mai Mai Kabido", wanamgambo wa jamii, miongoni mwa makumi ya makundi yanayoendesha mashambulizi mabaya mashariki mwa DRC.

Huko Nyamusengera, wakati wa doria katika mbuga hiyo karibu na mwambao wa Ziwa Edward ambalo ni mpaka na Uganda, walinzi wawili wa mazingira "walipigwa  risasi na kufariki kutokana na majeraha waliyoyapata", imesema taarifa hiyo.

"Leo asubuhi (Jumapili) tulisikia 'milio' ya risasi. Kundi la wawindaji haramu waliua kiboko na ili kujilinda waliwavizia walinzi wa mbuga hiyo," Kambale Muhindo, ofisa wa kituo cha Vitshumbi, kijiji cha wavuvi kilichopo Vitshumbi, amesema. kijiji kinachopatikana karibu kilomita 5 kutoka eneo la shambulio.

Mbali na wawili hao waliofariki, "walinzi sita wamejeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya Kikatoliki huko Vitshumbi," Blaise Kalisha, mtetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo, amesema.

Mnamo Mei 18, takriban kilomita sitini kaskazini zaidi, maafisa wanne wa mbuga hiyo, wakiwemo walinzi watatu, waliuawa katika shambulio la kuvizia dhidi ya "msafara wa mafundi (kutoka mbuga ya Virunga) waliopangiwa miradi ya maendeleo", kulingana na mamlaka, ambayo pia ilihusisha shambulio hilo wanamgambo wa Maimai.

Tangu 2020, walinzi kadhaa wameuawa wakati wa mashambulio au shambulio la kuvizia lililofanywa na makundi kadhaa yaliyojihami vilivyo na uadui wa Hifadhi ya Virunga. Walinzi wenye silaha ndio walengwa wakuu. Wanajaribu kuwazuia, wakati mwingine kwa njia za kijeshi, kufanya shughuli za uharibifu za wanyama na mimea ndani ya mipaka ya hifadhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.