Pata taarifa kuu

DRC: Mkutano wa upinzani mbele ya CENI

NAIROBI – Baada ya kukandamizwa kwa maandamano yao Jumamosi iliyopita, wapinzani Moïse Katumbi, Martin Fayulu, Matata Mponyo na Delly Sessanga walikuwa wameitisha tena maandamano mbele ya makao makuu ya tume ya taifa ya uchaguzi mjini Kinshasa dhidi ya kile wanachokiita uchaguzi usiohalali unaondaliwa nchini humo

Polisi nchini DRC walikabiliana na viongozi wa upinzani na wafuasi wao mbele ya ofisi za tume ya uchaguzi CENI Alhamis 25.05.23
Polisi nchini DRC walikabiliana na viongozi wa upinzani na wafuasi wao mbele ya ofisi za tume ya uchaguzi CENI Alhamis 25.05.23 © REUTERS - Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa wameshikana mikono, viongozi wa upinzani walijaribu kukaidi marufuku hiyo, lakini jeshi la polisi lenye nguvu lilikuwa tayari limetumwa kwenye Boulevard du 30-Juin kuwazuia. Maandamano hayo yalipigwa marufuku na mamlaka ya mijini.

Polisi walifunga barabara zinazoelekea katika tume ya uchaguzi alfajiri kabla ya kutawanya maandamano hayo muda mfupi mchana bila kutumia risasi wala mabomu ya machozi. Delly Sessanga anapinga.

“Polisi wanatumiwa na mamlaka kuingilia uhuru wetu na hatukubali hilo.’’Delly Sessanga kuhusu maandamano ya upinzani DRC.

00:07

Delly Sessanga kuhusu upinzani na polisi DRC

Miongoni mwa waandamanaji, Bienvenu Matumo ni mwanachama wa vuguvugu la wananchi wa Lucha.

“Nilikuja kushutumu mchakato wa uchaguzi ambao umekwama, ambao ni wa machafuko na ambao unatupeleka moja kwa moja kwenye uchaguzi ambao hautofanikiwa mnamo Desemba.’’ Bienvenu Matumo wa vuguvugu la wananchi wa Lucha

00:09

Bienvenu Matumo wa vuguvugu la wananchi wa Lucha

Polisi walipendekeza kwa waandamanaji kuunda ujumbe wa watu kumi ilikuingia katika tume ya  Ceni, pendekezo ambalo lilitupiliwa mbali na viongozi hao wa upinzani.

Kwa Moïse Katumbi, mchakato mzima haujakamilika, hata ukaguzi wa hivi karibuni wa daftari la uchaguzi uliofanywa na wataalam waliochaguliwa na Ceni.

"Hata sio ukaguzi huo. Ni tukio kamili. Hatuwezi kukagua rejista ya uchaguzi kwa siku tatu au nne. Ni upuuzi, tunataka uchaguzi wa kweli.’’ alisema Moïse Katumbi.

00:11

Moïse Katumbi kiongozi wa upinzani nchini DRC

Martin Fayulu amemtuhumu moja kwa moja na Denis Kadima, rais wa Ceni.

"Uchafuzi wa uchaguzi anaoutayarisha, tumeuelewa, umefichuka. Na unapaswa kuacha. Tutarejea tena Alhamisi ijayo, kila Alhamisi tutakuwa hapa.’’ alieleza Martin Fayulu.

00:13

Martin Fayulu kiongozi wa upinzani DRC

Akiwa ziarani nchini China rais Felix Tshisekedi amesema, wapinzani waandamani bila kuwa na dirá.

“Sijuwi ni nini wanataka, wametuhumu mambo kadhaa, wametuhumu CENI, wametuhumu mahakama ya kikatiba.” Alisema rais Felix Tshisekedi.

00:21

Felix Tshisekedi, Rias wa DRC kuhusu upinzani

Muda mfupi kabla ya saa moja jioni baada ya zaidi ya saa tatu za hali kama ilivyo sasa, polisi waliwatawanya waandamanaji hao kwa virungu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.