Pata taarifa kuu
USALAMA-MAANDAMANO

DRC: Maafisa kadhaa wa polisi wawekwa jela kufuatia maandamano ya Mei 20

Maafisa kadhaa wa polisi wako kizuizini tangu Jumamosi wiki iliyopita nchini DRC kwa kumpiga mtoto mdogo wakati wa maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani Moïse Katumbi, Martin Fayulu, Matata Mponyo na Delly Sessanga. Jumatatu alasiri, Rais Félix Tshisekedi amezuru watu waliojeruhiwa wakati wa maandamano hayo ambao wanalazwa katika hospitali kadhaamjini Kinshasa.

Maandamano ya upinzani yaliidhinishwa Mei 20, lakini yakatawanywa na polisi kwa kutoheshimu masharti yaliyowekwa na mamlaka.
Maandamano ya upinzani yaliidhinishwa Mei 20, lakini yakatawanywa na polisi kwa kutoheshimu masharti yaliyowekwa na mamlaka. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Washambuliaji, maafisa watatu wa polisi waliokamatwa tangu Jumamosi, wamepelekwa Jumatatu alasiri kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi kwa kukiuka sheria za walizojikubalisha kutii na shambulio la kukusudia.

Uongozi wa polisi unataka kutumia kesi hii kutuma ujumbe mkali kwa maafisa ambao watapatikana na hatia ya unyanyasaji na matumizi mabaya ya nguvu katika kutekeleza majukumu yao.

Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na Usalama ameiambia RFI kwamba maafisa wengine wa polisi waliotenda dhuluma wakati wa maandamano haya mawili wanasakwa. Ametangaza kesi dhidi ya maafisa hao katika siku zijazo.

Kuna maafisa 27 wa polisi waliojeruhiwa, wawili kati yao wako katika hali mbaya. Maafisa wa polisi ambao walikuwa bado wamelazwa hospitalini - karibu kumi - walitembelewa na Félix Tshisekedi, ziara ya ya kuwapa "faraja", kulingana na mkuu wa nchi.

Umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Marekani nchini DRC walitoa taarifa mbili siku ya Jumatatu kulaani "ukandamizaji mkali" dhidi ya maandamano ya upinzani na matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya waandamanaji, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo.

Rais Félix Tshisekedi alikwenda Jumatatu alasiri katika hospitali kadhaa kuwatembea majeruhi, akiwemo mtoto mdogo ambaye alipigwa na maafisa wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.