Pata taarifa kuu

Raia 6 wafariki nchini Congo baada ya kuporomoka kwa mgodi wa almasi.

Nairobi – Nchini DRC watu sita wameripotiwa kufa baada ya kuporoka kwa mgodi wa Amasi katika eneo la Diboko katikati mwa jimbo la Kasai .

Shughuli ya uokozi inaendelea katika mgodi wa Almasi nchini DRC
Shughuli ya uokozi inaendelea katika mgodi wa Almasi nchini DRC © LUIS CORTES/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Gaston Nkole ambaye ni Makamu wa gavana wa jimbo hilo ni kuwa waliofariki ni wachimba madini wasioà na vyeti vya uchimbaji na waliiongia kwenye mgodi huo kinyume na sheria.

Nchi hiyo ya Drc iliweka marufuku na sheria kadhaa kufuatilia swala la uchimaji madini ili kudumsiha usalama.Kuliungana na Gava,na huyo ni kuwa raia hao walikua wakifanya shughuli hiyo usiku.

Vile vile ameongeza kuwa sio kisa cha kwanza kuripotiwa nchini humo.  Mwaka 2019 watu zaidi ya 36 walifariki kayika mgodi wa shaba .Kwa mujibu wa taarifa kutoka  kampuni ya Glencore, wachimbaji hao walikuwa wakifanya kazi bila kibali katika Kampuni ya Kamoto Copper (KCC) katika eneo la kusini mashariki mwa Kongo wakati nyumba mbili zinazoangalia eneo la uchimbaji ziliporomoka.

Ajali za uchimbaji madini ni za kawaida nchini DRC, ambapo maelfu ya wachimbaji wasio na vifaa rasmi hutafuta almasi, dhahabu na madini ya thamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.