Pata taarifa kuu

Kiir: Pande zinazozozana Sudan zakubali kusitisha mapigano kwa siku 7

NAIROBI – Pande zinazohasiana nchini Sudan zimekubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba kuanzia Mei 4.

Upande wa kushoto, mkuu wa majeshi ya Sudan, Jenerali al-Burhan na upande wa kulia, kiongozi wa kikosi cha RSF Jenerali Hemedti.
Upande wa kushoto, mkuu wa majeshi ya Sudan, Jenerali al-Burhan na upande wa kulia, kiongozi wa kikosi cha RSF Jenerali Hemedti. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, wizara ya mambo ya nje ya Juba imezungumzia kuafikiwa kwa makubaliano hayo, na kuibua matumaini ya kukomesha wiki kadhaa za umwagaji damu.

Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, kiongozi wa kundi la RSF, Mohamed Hamdan Daglo, wamekubaliana kusitisha mapigano kuanzia Mei 4 hadi Mei 11, imesema taarifa.

Mamia ya watu wameuawa katika mapigano hayo yaliyoanza Aprili 15, huku maelfu wakijeruhiwa katika mapigano kati ya majenerali hao wawili wakati huu nchi mbalimbali za kigeni zikiongeza juhudi za kuwahamishwa raia wao nchini humo. 

Taarifa hiyo kutoka Juba imeendelea kusema kuwa Burhan na Daglo, wamekubaliana kuwatuma wawakilishi wao kuhudhuria mazungumzo ya amani yatakayofanyika katika eneo watakalokubaliana wao.

Kiir amezungumza na Burhan na Daglo kama sehemu ya mpango wa kambi ya kanda ya Afrika Mashariki IGAD, ambayo imekuwa ikishinikiza kukomesha mapigano, ikitoa wito wa Umoja wa Afrika na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.