Pata taarifa kuu

Kenya: Serikali kuunda tume ya uchunguzi kuhusu makanisa

NAIROBI – Siku chache kupita tangu viongozi kadhaa wa kidini kukamatwa kwa tuhuma za kutoa mahubiri potofu pamoja na kuhusishwa na mauaji ya waumini wao, rais wa Kenya, William Ruto, amesema ataunda tume maalumu kuchunguza yanayoendelea na kutoa mapendekezo ya nini cha kufanyika.

Maofisa wa polisi nchini Kenya wanaendelea na uchunguzi baada ya miili zaidi ya mia moja kufukuliwa katika shamba la mhubiri wao
Maofisa wa polisi nchini Kenya wanaendelea na uchunguzi baada ya miili zaidi ya mia moja kufukuliwa katika shamba la mhubiri wao AP
Matangazo ya kibiashara

Kauli yake ameitoa wakati huu polisi ikiendelea kumshikilia muhubiri tata Paul Mackenzie, ambaye katika eneo la shamba lake la Shakahola, miili ya watu zaidi ya 100 ilipatikana katika makaburi 23.

“Nchi yake Kenya ni nchi inayomcha Mungu na kuna watu wengine ambao wanataka kutumia dini kuharibu na kuumiza watu wengine.” alisema rais William Ruto.

00:42

Rais wa Kenya William Ruto kuhusu wachungaji feki

Wafuasi wa dhehebu la mhubiri huyo wamethibitisha kufariki baada ya kuagizwa na kiongozi huyo wa dini kufa hadi kufa iliwamuone Kristo kwa haraka. Waumini wa kanisa hilo wamedai kuwa walilazimika kufunga kama sehemu ya kufuata mafundisho yake.

Mnamo 2017 na tena 2018 kiongozi huyo wa dini ambaye sasa anashikiliwa na maofisa wa polisi alikamatwa kwa kuhimiza watoto wasiende shule kwani alidai elimu "haitambuliki katika Biblia".

Maofisa wa usalama nchini Kenya wanaendelea na juhudi za uokozi zaidi katika shamba la mchungaji mwenye utata baada ya wafuasi wake kufariki
Maofisa wa usalama nchini Kenya wanaendelea na juhudi za uokozi zaidi katika shamba la mchungaji mwenye utata baada ya wafuasi wake kufariki AP

Pia amewahimiza akina mama kuepuka kutafuta matibabu wakati wa kujifungua na kutowachanja watoto wao.

Mengi ya mahubiri ya Mchungaji Mackenzie yanahusiana na utimizo wa unabii wa Biblia kuhusu Siku ya Hukumu.

Maofisa wa upelelezi wanaeleza kuwa wengi wa waliofariki ni watoto na wanawake. Wafuasi waliookolewa katika shamba la mchungaji huyo walipatikana miili yao ikiwa imedhoofika zaidi.

Wafuasi wa kanisa la mchungaji Paul Makenzie wanadaiwa kuzikwa katika makaburi kwenye shamba la mhubiri huyo
Wafuasi wa kanisa la mchungaji Paul Makenzie wanadaiwa kuzikwa katika makaburi kwenye shamba la mhubiri huyo AP

Mwishoni wa wiki iliyopita hhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre and Church, kupitia mawakili wake, amekiri kuwa watu 15 wamekufa wakati wakitafuta ushauri wake wa kiroho kanisani mwake, katika kipindi cha miezi kumi na tatu, tangu kanisa hilo lilipoanzishwa.

Kupitia kwa mawakili wake Cliff Ombeta, Danstan Omari na Shadrack Wamboi, muinjilisti Odero walisema kuwa waliofariki, walienda kutafuta msaada wake wa kiroho wakiwa katika hali mbaya.

Wakili Omari, alisema kanisa la mteja wao lina sera, ambapo wale ambao wanaugua sana, lazima waandamane na jamaa zao, na iwapo watakosa kufanya hivyo hawatahudumiwa kupitia maombi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.