Pata taarifa kuu

Senegal: Sonko kushtakiwa kwa madai ya ubakaji mwezi Mei

NAIROBI – Wakili El Hadji Diouf, ambaye anamuwakilisha kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, amesema mteja wake atakabiliwa na mashtaka ya madai ya ubakaji.

Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani wa Senegal, Machi 8, 2021.
Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani wa Senegal, Machi 8, 2021. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii itasikilizwa Mei 16, na matamshi ya wakili yake, yanathibitisha ripoti za awali za vyombo vya habari.

Sonko ambaye katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019 aliibuka wa tatu, ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na ametangaza kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Mkaguzi huyu wa zamani wa ushuru, anadaiwa kumbaka mfanyakazi wa saluni alikokuwa ameenda kufanyiwa masaji, ambapo mwezi Januari, jaji alihamisha kesi hiyo kwa mahakama ya jinai.

Sonko, mwenye umri wa miaka 48, amekanusha shtaka hilo na kusema yeye ni mwathirika wa njama ya Rais Macky Sall ambaye anadai anataka asigombee urais mwaka ujao.

Sonko na Sheria

Mnamo Machi 2021, Sonko alikamatwa lakini hatua hiyo ilisababisha kuzuka kwa ghasia za siku kadhaa ambapo takriban watu 12 waliuawa. Mwezi huo huo Soko alihukumiwa kifungo cha miezi miwili kwa kumkashifu Waziri wa utalii Mame Mbaye Niang, mwanachama wa chama cha Sall.

Wafuasi wa mpinzani wa Senegal Ousmane Sonko waliandamana kwa maelfu mjini Dakar mnamo Machi 14, 2023..
Wafuasi wa mpinzani wa Senegal Ousmane Sonko waliandamana kwa maelfu mjini Dakar mnamo Machi 14, 2023.. © Zohra Bensemra / Reuters

 

Chama cha Sall kinamshutumu Sonko kwa kutaka kuilemaza Senegal na kuongeza hasira mitaani ili kuepuka haki.

Rais Sall hajaweka wazi nia yake kweney uchaguzi ujao wa urais lakini anakanusha madai kuwa itakuwa kinyume cha katiba kwake kugombea kwa muhula mwingine.

Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameelezea wasiwasi wake kuhusu vikwazo vya uhuru wa kukusanyika na kujieleza nchini Senegal na kumtaka Sall kutowania muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.