Pata taarifa kuu

Matukio ya dhulma za kijinsia yaongezeka Mashariki ya DRC

NAIROBI – Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, pamoja na Umoja wa mataifa yamesema kuwa visa vya dhuluma za kimapenzi  vinaendelea kuongezeka hususan karibu na kambi za wakimbizi, maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo.

Wanawake kutoka kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Kitchanga wanasikiliza Margot Wallstrom
Wanawake kutoka kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Kitchanga wanasikiliza Margot Wallstrom Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya umoja wa mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu OCHA ni kuwa Mwaka uliopita, visa 120 viliripotiwa, huku makundi ya waasi yakidaiwa kuhusika.

Bruno Lemarquis, ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa, anayehusika na misaada ya kibinadamu.

Mfano ulio hai ni kulipuka kwa matukio ya ubakaji mwezi hadi mwezi, siku hadi nyingine, ambayo imeorodheshwa vizuri katika vituo vya waliokimbia makwao karibu na Goma, Amesema Lemarquis.
00:35

Bruno Lemarquis, ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Baadhi ya mashirika kama Bon Dieu dans la Rue, na IRC yanajaribu kuwasaidia waathiriwa wa ubakaji, kama anavyoeleza Amani Linda, kutoka shirika la Bon dieu dans la Rue.

Hapo ndani ya kambi wameona shida kali sana, hawana chakula ndio maana wanaenda kutafutisha chakula kwa njia nyingi sana ili watoto wakule, Amesema Linda.
00:14

Amani Linda, kutoka shirika Bon dieu dans la Rue

Umoja wa Mataifa, unahusisha visa hivyo na utovu wa usalama Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.