Pata taarifa kuu

Mapigano yanaendelea nchini Sudan, mamia ya raia wauawa

Raia zaidi ya mia moja wameuawa nchini Sudan ambapo milio ya risasi na milipuko ya mabomu imeongezeka siku ya Jumatatu mjini Khartoum, katika siku ya tatu ya mapigano kati ya jeshi na kikosi chenye nguvu cha wanamgambo, vikosi viwili vinavyoongozwa na majenerali wawili hasimu wanaowania madaraka.

Tangu Jumamosi, mapigano ya silaha nzito hayajakoma na jeshi la anga linalenga mara kwa mara, hata katikati ya Khartoum, makao makuu ya FSR, wanamgambo wa zamani kutoka vita katika eneo la Darfur ambao wamekuwa wasaidizi rasmi wa jeshi.
Tangu Jumamosi, mapigano ya silaha nzito hayajakoma na jeshi la anga linalenga mara kwa mara, hata katikati ya Khartoum, makao makuu ya FSR, wanamgambo wa zamani kutoka vita katika eneo la Darfur ambao wamekuwa wasaidizi rasmi wa jeshi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumamosi, mji mkuu unaendelea kukumbwa na mapigano. Wakazi wake wamezingirwa na hawatoki katika nyumba zao, huku wakiwa hawana maji ya bomba au umeme kwa sehemu kubwa, wakiingiliwa na hofu kwa kila shambulio jipya la anga au mizinga. Raia 97 wameuawa, karibu nusu mjini Khartoum, kulingana na chama cha rasmi cha madaktari, na "dazeni" za wapiganaji wameuawa katika mapigano haya. Kambi hizi mbili hazijawahi kutoa taarifa kuhusuwapiganaji wao ambao wameuawa tangu vita hii kuanza.

Mjini Khartoum, wanajeshi pekee na magari ya kijeshi ndio huzunguka, maduka machache ya mboga yaliyofunguliwa yameonya kwamba yatadumu kwa siku chache tu ikiwa hakuna lori litawasili. Hospitali zinazopokea majeruhi zinakabiliwa na uhaba wa damu na vifaa. Baada ya Umoja wa Nchi za Kiarabu na Umoja wa Afrika, Marekani na Uingereza zilitoa wito siku ya Jumatatu wa"kusitishwa mara moja" kwa ghasia.

Mzozo huo ulikuwa umefichwa kwa wiki kadhaa kati ya mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, kiongozi mkuu wa nchi, na naibu wake, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama "Hemedti", mkuu wa vikosi vya msaada wa haraka (FSR), ambao kwa pamoja waliwaondoa raia mamlakani wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba 2021.

Tangu Jumamosi, mapigano ya silaha nzito hayajakoma na jeshi la anga linalenga mara kwa mara, hata katikati ya Khartoum, makao makuu ya FSR, wanamgambo wa zamani kutoka vita katika eneo la Darfur ambao wamekuwa wasaidizi rasmi wa jeshi. Siku ya Jumapili jioni jeshi lilihakikisha kwamba hali ilikuwa "tulivu" huku FSR ikisema "wako njiani kushinda vita".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.