Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Niger: Mwanaharakati ahukumiwa kifungo cha miezi tisa jela

Mwanaharakati wa mashirika ya kiraia nchini Niger Abdoulaye Seydou amehukumiwa siku ya Ijumaa kifungo cha miezi tisa jela kwa "kusambaza data zinazoweza kuhatarisha usalama wa taifa".

Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 waliuawa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021.
Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 waliuawa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021. AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

Bw. Seydou, mratibu wa vuguvugu la M62, alikamatwa mwishoni mwa mwezi Januari na kuwekwa kizuizini. shirika lake vilishutumu vikosi vya ulinzi na usalama kwa mauaji ya raia kwa kulipiza kisasi shambulio la wanajihadi mnamo Oktoba 24, 2022 dhidi ya kituo cha polisi huko Tamou (kusini).

Baada ya shambulio hili, jeshi la Niger lililipiza kisasi na kuwaua "washambuliaji" saba kwenye eneo la siri kunakochimwa dhahabu. Upinzani wa kisiasa na mashirika ya kiraia yalikuwa yalidai kwamba mashambulizi haya yalisababisha vifo vingi.

Kulingana na mwendesha mashtaka wa umma Chaïbou Moussa, uchunguzi umeonyesha kwamba "watu wasiojulikana" walienda kwenye eneo hii kunakochimbwa dhahabu, "wakachoma moto maduka na vibanda vilivyotumika kama nyumba" na Bw. Seydou alikamatwa kwa "kuhusika katika uchomaji moto" na "kutengeeza na kusambaza data zenye lengo la kuhatarisha usalama wa taifa".

Tukio hili lilikuwa na "lengo pekee la kuunda ushahidi wa uwongo ili kulishtumu" jeshi na "kutoa sifa kwa nadharia ya mauaji" yaliyotekelezwa na jeshi, amesema mwendesha mashitaka. Bw. Seydou amehukumiwa siku ya Ijumaa kifungo cha miezi tisa jela na faini ya faranga milioni moja za CFA (sawa na euro 1,524). Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, shirika la kimataifa la Amnesty International imetaka "kuachiliwa bila masharti" kwa mwanaharakati huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.