Pata taarifa kuu

Dakar yachunguza wahamiaji walioteweka Tunisia

Dakar inmeanza zoezi la kuitambua miili ya raia 'ishirini' wa Senegal ambao walifariki baada ya boti waliokuemo kuzama mwishoni mwa mwezi Machi katika kwenye pwani ya Tunisia, taarifa rasmi imesema hivi punde.

Wengi wa wahamiaji wengi wa Kiafrika huwasili Tunisia ili kujaribu kuingia Ulaya kwa njia ya baharini.
Wengi wa wahamiaji wengi wa Kiafrika huwasili Tunisia ili kujaribu kuingia Ulaya kwa njia ya baharini. REUTERS/Jesus Moron
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Senegal ulikwenda SFAX, katikati mwa mashariki mwa Tunisia mahali pa kuanzia boti iliyofanya ajali ilianza safari yake, kwa "dhamira ya kutambua miili", kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje.

Kwa sasa, "hakuna miili iliyoondolewa majini na walinzi wa pwani ya Tunisia ambayo ni raia wetu" waliotoweka baada ya ajali hiyo ya boti iliyotokea "usiku wa Machi 23 kuamkia 24 katika Bahari ya Mediterania", imebaini wizara, ambayo haielezi idadi ya miili. Ubalozi wa Senegal huko Tunis "utaendelea kuwasiliana na mamlaka ya (Tunisia) na shirika la Ilani nyekundu la Tunisia kwa kufuata zoezi hili la kuondoa miilli majini na utambulisho wa wahanga," imeongezea taarifa.

Wahamiaji kadhaa walikufa maji katika mfululizo wa visa vya kuzama kwa boti na wengine walikosekana tangu hotuba ya kibaguzi ya Rais Kais Saed juu ya uhamiaji haramu, mnamo Februari 21. Baada ya hotuba hii, sehemu muhimu ya Raia 21,000 kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara waliorodheshwa rasmi nchini Tunisia, wengi wakichukuliwa kama wahamiaji haramu, walipoteza kazi mara moja, kinyume cha sheria, na malazi yao, kwa sababu ya kampeni dhidi ya wahamiaji haramu.

Wahamiaji wengi wa Kiafrika huingia Tunisia kisha kujaribu kuhamia Ulaya kwa kutumia njia ya baharini, baadhi ya sehemu za pwani ya Tunisia ziko chini ya kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampusa. Katikati ya mwezi Machi, Dakar ilirudisha watu 76 kutoka Tunisia na Libya baada ya maneno ya kiongozi wa Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.