Pata taarifa kuu

Ukame: Tunis yaweka vikwazo juu ya matumizi ya maji

Mamlaka ya Tunisia siku ya Ijumaa imetangaza vikwazo vya usambazaji na matumizi ya maji ya kunywa katika nchi hiyo iliyokumbwa na ukame ili kuhifadhi akiba ya chini ya mabwawa yake.

Moja ya maenro ya mji mkuu wa Tunisia, Tunis.
Moja ya maenro ya mji mkuu wa Tunisia, Tunis. © Éric Bataillon/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuzingatia mzunguko wa miaka ya ukame, ambao umekuwa na athari mbaya kwa hifadhi ya mabwawa hadi kufikia kiwango (cha udhaifu) kisicho na kifani," Wizara ya Kilimo, Rasilimali za Maji na Uvuvi imeamua kupiga marufuku matumizi ya maji ya kunywa katika umwagiliaji wa kilimo na maeneo ya kijani kibichi, kusafisha mitaa na maeneo ya umma, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Inabainisha kuwa hatua hizi zitakuwa "za muda". Kwa kukosekana kwa mvua, mabwawa thelathini nchini yanayotumika kwa umwagiliaji lakini pia kwa usambazaji wa maji ya kunywa yanaonyesha viwango vya kutisha kwa ukosefu wa maji. Hakuna hata moja linalofikia theluthi moja ya kiwango cha juu, kulingana na takwimu rasmi.

Tunisia inapitia mwaka wake wa tano mfululizo wa ukame ambao unakumba maeneo yenye ukame kama vile Kasserine (katikati-magharibi) na Gabes (kusini) ngumu zaidi kuliko kawaida, lakini pia kaskazini-magharibi na hali ya hewa yake ya joto zaidi.

Kwa raia, ambao tayari wamekumbwa na mzozo mkubwa wa kijamii na kiuchumi na kisiasa, usambazaji wa maji ya kunywa pia utakadiriwa kwa muda fulani na kulingana na mfumo wa mzunguko hadi mwisho wa mwezi Septemba. Kwa wiki iliyopita, mamlaka ya Maji (Sonede) imeanza kutekeleza, bila tangazo la awali, kukata maji huko Tunis na katika miji mingine mikubwa kama vile Sfax na Hammamet.

"Kupunguzwa huku kutafanywa kwa ujumla kwa nchi nzima," afisa wa Sonede ameliambia shirika la habari la AFP, kwa sharti la kutotajwa jina. Hali hii ya kutisha itakuwa na madhara kwa kilimo, rasilimali kuu ya kiuchumi ya nchi, inayowakilisha takriban 10% ya Pato la Taifa. Nchini Tunisia, rasilimali nyingi za maji huenda kwenye umwagiliaji na kilimo.

Akihojiwa na redio, msemaji wa Muungano wa Kilimo na Uvuvi wa Tunisia (Utap), Anis Karbach, alitabiri uzalishaji "mbaya" wa nafaka, uliopungua hadi quintals milioni 2 mwaka huu, yaani chini ya theluthi moja ya mwaka uliopita. Hii itafanya Tunisia kutegemea zaidi uagizaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.