Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Côte d'Ivoire: Rais wa zamani Bédié atoa wito wa umoja katika chama chake

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire, Henri Konan Bédié, ambaye sasa ni mpinzani, siku ya Alhamisi ametoa wito kwa wanachama wa chama chake kuungana ili kushinda uchaguzi ujao wa urais mwaka 2025, baada ya kujitoa katika wiki za hivi karibuni kwa baadhi ya makada wa chama hicho.

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Henri Konan Bédié.
Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Henri Konan Bédié. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

"Tunahitaji umoja na mshikamano ndani ya safu zetu ili kushinda vita hivi vijavyo", ametangaza Bw. Bédié, katika hotuba ya takriban dakika thelathini, wakati wa kongamano la lisilo kuwala kawaida la Chama cha Demokrasia cha Côte d'Ivoire (PDCI).

Wito huu wa umoja unaangazia kasoro katika wiki za hivi karibuni za baadhi ya makada wa chma cha PDCI, kama vile mkuu wa zamani katika ofisi ya Bw. Bédié, Narcisse N'Dri, ambaye alijiunga na chama tawala.

Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 88 pia alidokeza kwamba muungano unaweza kutengenezwa na vyama vingine kwa ajili ya uchaguzi ujao. "Vikosi viwili vinapounganishwa, ufanisi wao ni maradufu. Kuungana na kudhamiria, tuunganishe nguvu zetu zote", amezindua mbele ya zaidi ya wajumbe elfu moja.

Viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa wameketi katika safu ya mbele: makada kutoka chama cha rais mwingine wa zamani, Laurent Gbagbo, Mke wa Rais wa zamani Simone Gbagbo, au hata Charles Blé Goudé. Wote walishangiliwa na umaati wawatu, pamoja na mwakilishi wa Ubalozi wa Urusi.

Katika hotuba yake, Henri Konan Bédié pia alitoa kauli kali kuhusu Côte d'Ivoire. "Raia wet wanateseka. Umaskini haujawahi kutokea, mfumo wetu wa elimu unashuka," amesema, huku wawakilishi wa chama tawala walioalikwa kwenye kongamano hilo wakizomewa na baadhi ya wafuasi wa chamach PDCI.

Bw. Bédié, hata hivyo, alihakikisha kuwasiliana na Rais Alassane Ouattara "kushiriki katika mazungumzo ya wazi na ya dhati kwa manufaa ya amani ya kudumu". Uchaguzi wa manispaa na mikoa utafanyika mwezi Septemba 2023. Uchaguzi ujao wa urais utafanyika mwaka wa 2025.

Henri Konan Bédié, ambaye alitawala Côte d'Ivoire kuanzia mwka 1993 hadi 1999, hataki kuwa mgombea wa PDCI katika uchaguzi huu. Atakuwa na umri wa miaka 91. Wanachama wengine wa chama chake pia wameelezea nia yao ya kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho, kama vile Waziri wa zamani wa Biashara Jean-Louis Billon.

Chama cha zamani cha PDCI kilikuwa madarakani kuanzia 1960, wakati wa uhuru wa Côte d'Ivoire, hadi mwaka 1999. Wakati akishirikiana na Rais Alassane Ouattara aliyechaguliwa mwaka 2010, alirejea tangu 2018 kwa upinzani ambako alikaribia wafuasi wa Laurent Gbagbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.