Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Senegal: Hali ya wasiwasi yatanda usiku wa kuamkia kesi ya Ousmane Sonko

Licha ya kupigwa marufuku na mamlaka, upinzani wa Senegal umeendeleza wito wake wa kuandamana, Jumatano hii, Machi 29 mchana huko Dakar, kupinga kesi ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, aliyefunguliwa mashitaka na Waziri wa Utalii kwa kumharibia jina. Upinzani unabaini kwamba mamlaka inatumia mahakama kuukandamiza.

Maafisa wa polisi wa Senegal, wakipiga kambi karibu na Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop huko Dakar, Jumatano hii, Machi 29, 2023.
Maafisa wa polisi wa Senegal, wakipiga kambi karibu na Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop huko Dakar, Jumatano hii, Machi 29, 2023. © AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Dakar, Charlotte Idrac

Karibu na Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop (UCAD), ambapo kulitarajiwa kuanza kwa maandamano haya yaliyopigwa marufuku, polisi na wanafunzi walijikuta uso kwa uso, mara kwa mara, kurusha mawe na mabomu ya machozi, hata kama mapema jioni utulivu ulikuwa umerejea, angalau kwa muda.

Maafisa weni wa polisi wametumwa katika maeneo kadhaa muhimu ya jiji, karibu na chuo kikuu na karibu na nyumba ya Ousmane Sonko, katika wilaya ya Cité Keur Gorgui.

Mapema mchana, maafisa na wabunge kutoka muungano wa upinzani, Yewwi Askan Wi, ambao ulitaka kufanya mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya PRP, Chama cha Upyaji na Maendeleo, walitawanywa, tena kwa mabomu ya machozi.

Maandamano haya yalikuwa yamepigwa marufuku, hasa kwa vitisho vya kweli vya kuhatarishausalama, kulingana na mkuu wa mkoa. Sababu hiyo ilipelekea kupigwa marufuku kwa maandamano yaliyopangwa kufanyika Alhamisi huko Dakar, hata kama maandamano katika maeneo mengine yameidhinishwa.

Alhamisi hii, Machi 30, inafunguliwa kesi - iliyo hatarini kwa mustakabali wa kisiasa - wa Ousmane Sonko, na kuzua hofu ya kutokea machafuko mapya.

Shule zimefungwa kote nchini, likizo zimeletwa mbele. Mjini Dakar, maduka na benki yamefungwa nna safari za mabasi kutoka kwa kampuni ya kitaifa zimesimamishwa.

Utawala na upinzani wamekuwa zikionyesha azma yao kwa wiki kadhaa katika mvutano huu, na katika maandalizi ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika katika kipindi kiichozidi mwaka mmoja mnamo Februari 2024.

Kiogozi wa chama cha Pastef ni mgombea, lakini utaratibu huu unaweza kumzuia kuelekea kwenye uchaguzi. Kesi yake, baada ya kufutwa kazi mara tatu, inazua hofu ya kutokea machafuko mapya, kama ilivyokuwa wakati kesi hiyo ilisikilizwa hapo awali mnamo Machi 16.

Kwa upande wa upinzani, wanatetea mapambano ya "uhuru" na dhidi ya "utumiaji wa vyombo vya sheria". Kwa upande wa utawala, dhamira inayoonyeshwa ni kutetea “utaratibu wa umma na usalama wa watu na mali”.

Kesi hii itakuwa hatua mpya katika mvutano, chini ya mwaka mmoja kutoka tarehe ya mwisho ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.