Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Senegal: Mtu mmoja afariki Casamance katika makabiliano kati ya wapinzani na polisi

Mtu mmoja amefariki Jumatatu huko Casamance, kusini mwa Senegal, kayika makabiliano kati ya wafuasi wa mpinzani Ousmane Sonko na polisi, shirika la habari la AFP limeripoti likinukuu vyanzo vya ndani na kiutawala.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, katika makabiliano na vikosi vya usalama kabla ya kufikishwa mahakamani kwa kiongozi wa chama cha Pastef katika kesi ya kumkashifu huko Dakar, Senegal Machi 16, 2023.
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, katika makabiliano na vikosi vya usalama kabla ya kufikishwa mahakamani kwa kiongozi wa chama cha Pastef katika kesi ya kumkashifu huko Dakar, Senegal Machi 16, 2023. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Tangu Machi 16, siku ya kuanza kwa kesi ya Bw Sonko aliyeshtakiwa kwa kashfa na Waziri wa Utalii Mame Mbaye Niang, makabiliano yameripoitwa kati ya makundi ya vijana na vikosi vya usalama katika miji kadhaa nchini. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 30.

Katika mji wa Bignona, ngome ya Bw. Sonko yapata kilomita 30 kutoka Ziguinchor, mji mkuu wa Casamance, 'mtoto amepigwa risasi' na polisi, Yankhoba Diémé ameliambia shirika la habari la AFP.

Makabiliano yalizuka na polisi wakati "vijana walipojitokeza wenyewe kuandamana barabarani" kupinga mamlaka, amesema Bw. Diémé, mwanachama wa chama cha Bw. Sonko. Kifo cha mtu mmoja huko Bignona kilithibitishwa na afisa wa utawala ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina.

"Ndiyo. Mt mmoja alifariki kufuatia maandamano," ameliambia shirika la habari la AFP. Waziri Niang anamshtaki Bw Sonko kwa kumkejeli, kumtusi na kughushi nyaraka zisizo halali. Anamtuhumu kwa kutangaza kuwa ameteuliwa na ripoti kutoka kwa taasisi ya udhibiti wa usimamizi wake wa mfuko wa kuajiri vijana katika kilimo.

Kilicho hatarini ni zaidi ya sifa ya waziri. Maandishi yanayotumika yanatoa fursa ya kuondolewa kwenye orodha za wapiga kura, na kwa hivyo kutostahiki, katika baadhi ya visa vya kutiwa hatiani. Kwa hivyo Bw. Sonko ana hatari ya kutangazwa kuwa hafai kwa uchaguzi wa urais wa 2024. Yeye na wafuasi wake wanalani mahakama kushinikizwa na mamlaka ili kumuondoa katika siasa.

Mnamo Machi 2021, kuhojiwa kwa Bw. Sonko katika kesi ya madai ya ubakaji na kukamatwa kwake akiwa njiani kufikishwa kortini kulichangia kuchochea ghasia mbaya zaidi kwa miaka mingi nchini humu inayojulikana kama kisiwa adimu cha utulivu katika eneo lenye matatizo. Watu zaidi ya kumi na mbili walifariki wakati huo. Kesi ya madai ya ubakaji, ambayo haijahukumiwa kwa sasa, pia inaleta tishio la uwezekano wa kutostahiki kwa Bw. Sonko katika uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.