Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Raia kadhaa wauawa Ituri, mapigano yarindima kati ya FARDC na M23

Takriban raia 20 waliuawa siku ya Jumamosi katika mashambulizi mawili tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo mapigano pia yalianza kati ya jeshi na waasi wa M23, duru za ndani zimesema siku ya Jumapili.

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mikoa ya mashariki mwa DRC imekumbwa na ghasia kutoka kwa makumi ya makundi yenye silaha kwa takriban miaka 30.

 

Takriban raia 20 waliuawa siku ya Jumamosi katika mashambulizi mawili tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo mapigano pia yalianza kati ya jeshi na waasi wa M23, duru za ndani zimesema siku ya Jumapili.

Katika mkoa wa Ituri, wanamgambo wa CODECO, ambao wanadai kulinda kabila la Lendu dhidi ya kabila la Hema, wanatuhumiwa kushambulia vijiji vitano katika eneo la Mahagi Jumamosi asubuhi.

"Hadi sasa tumehesabu watu 15 waliofariki, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee," Arnold Lokwa, mkuu wa kundi la vijiji la Panduru, ameliambia shirika la habari la AFP.

Katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, waasi wa ADF (Allied Democratic Forces) wenye mfungamano na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS), ndio ambao wanatuhumiwa kuwaua takriban watu tisa katika kijiji cha Nguli, katika eneo la Lubero.

Wahanga "waliuawa silaha za jadi, mapanga na visu", mtu wa kumi alijeruhiwa vibaya na watoto wawili hawajulikani walipo", Kambale Kamboso, kiongozi wa kijiji hicho ameliambia shirika la habari la AFP.

Hapo awali waasi wa Uganda ambao wengi wao ni Waislamu , ADF wamekita mizizi tangu katikati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambapo wanashutumiwa kwa mauaji ya maelfu ya raia.

Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, lakini kusini zaidi, mapigano pia yalianza tena Jumamosi kati ya jeshi na waasi wa M23 katika eneo la Masisi, kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, baada ya siku chache za tulivu.

Katika taarifa, jeshi limeshutumuwaasi hao kwa kushambulia angalau ngome zake sita na kufanya 'ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji mapigano'.

Wakaazi waliohojiwa kwa njia ya simu wameripoti mapigano siku ya Jumamosi jioni huko Bihambwe, karibu na mji wa madini wa Rubaya.

M23 ("kundi lililoundwa Machi 23") ni waasi ambao wengi wao ni Watutsi, wanaoungwa mkono na Rwanda kulingana na Kinshasa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, ambao wameteka maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini kwa mwaka mmoja.

Baada ya matangazo kadhaa ya usitishaji mapigano ambao haukutekelezwa, usitishaji mapigano ulipaswa kuanza Machi 7 lakini haukutekelezwapia.

Mapigano hayo hata hivyo yamesimama siku chache wiki hii, huku M23 wakiondoka katika vijiji ambako wanajeshi wa Burundi kutoka katika kikosi kilichotumwa katika ukanda huo na Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) walitumwa.

Mikoa ya mashariki mwa DRC imekumbwa na ghasia kutoka kwa makumi ya makundi yenye silaha kwa takriban miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.