Pata taarifa kuu

Nigeria: Raia wamepiga kura kuwachagua wabunge na magavana

NAIROBI – Mamilioni ya wapiga kura nchini Nigeria, kuwachagua Magavana na wabunge wa majimbo mbalimbali, wiki kadhaa baada ya chama tawala kushinda uchaguzi wa urais.

Raia nchini Nigeria wanapiga kura kuwachagua wabunge na magavana
Raia nchini Nigeria wanapiga kura kuwachagua wabunge na magavana eNCA
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura, vilifunguliwa saa mbili na nusu asubuhi, saa za Abuja na kufungwa saa nane na nusu mchana, na kufuatiwa na zoezi la kuanza kuhesabu kura.

Kwa kiasi kikubwa, vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati, lakini majimbo mengine yalishuhudia ucheleweshwaji wa watu kupiga kura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa urais.

Kuna majimbo 36 nchini Nigeria, lakini ushindani mkali unatarajiwa katika jimbo la Lagos, jiji kuu la kiuchumi nchini humo, Kati ya mgombea wa chama tawala Babajide Sanwo-Olu kutoka APC, Gbadebo Rhodes-kutoka chama cha Leba na Olajide Adediran kutoka chama kikuu cha upinzani PDP.

Magavana nchini Nigeria, ni viongozi wenye mamlaka makubwa kwenye majimbo yao, na hudhibiti bajeti ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na baadhi ya mataifa ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.