Pata taarifa kuu

Burundi: Wanaharakati watano wa haki za binadamu bado wanazuiliwa

NAIROBI – Mahakama ya rufaa nchini Burundi, imethibitisha kuendelea kushikiliwa kwa wanaharakati watano wa haki za binamu, akiwemo Sonia Ndikumasabo,rais wa chama cha Mawakili wanawake nchini humo, ambaye pia aliwahi kuhudulu kama naibu Mwenyekiti wa Tume huru ya kutetea haki za binadamu. 

Nembo ya shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch
Nembo ya shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch Human Rights Watch
Matangazo ya kibiashara

Walikamatwa tarehe 14 mwezi Februari kwa madai ya kuhatarisha usalama na uchumi wa nchi hiyo. 

Mashirika ya kutetea haki za binadamu kama Human Rights Watch na Amnety International yamelaani kuzuiwa kwa wanaharakati hao. 

Clémentine de Montjoye, ni mtafiti kutoka Human Rights Watch barani Afrika. 

“Nafasi kidogo iliyoachwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi nchini Burundi, itatoweka, hasa baada ya ukamataji huu kuja baada ya kufungwa kwa mwanahabari Floriane IRANGABIYE na kukatisha matumaini baada ya kuachiwa kwa mtetezi wa haki za binadamu Tony Germain.”amesema Clémentine de Montjoye.

Aidha amesisitiza kuwa inasikitisha kuwa yote haya yanajiri baada ya IRANGABIYE, kufungwa jela miaka 10 kwa kuhatarisha usalama wa taifa suala ambalo ni ukiukwaji wa haki za kujieleza na kupata hukumu yenye haki. 

Tangu aingie madarakani mwaka wa 2020, Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, ametofautiana kati ya dalili za uwazi wa utawala, ambao unasalia chini ya ushawishi wa "majenerali" wenye nguvu na udhibiti thabiti wa mamlaka unaoonyeshwa na ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unashtumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Alimrithi Pierre Nkurunziza, aliyefariki mwaka 2020, ambaye alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma tangu mwaka 2005.

Burundi, ambayo haina bahari katika eneo la Maziwa Makuu, ndiyo nchi maskini zaidi duniani kwa pato kwa kila mtu kulingana na Benki ya Dunia, ambayo inabaini kuwa 75% ya wakazi wake milioni 12 wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.