Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: Kiir na Machar kufanya mazungumzo

NAIROBI – Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na makamu Wake Riek Machar, hivi leo wanatarajiwa kuwa na mazungumzo yanayolenga kuzungumzia hatua ya hivi karibuni ya Kiir, kumfuta kazi mke wa Machar aliyekuwa anahudumu kama waziri wa ulinzi.

Makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar na rais Salva Kiir mjini  Juba.
Makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar na rais Salva Kiir mjini Juba. ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir pia alimfuta kazi waziri wa mambo ya ndani pamoja na waziri wake wa mambo ya nje, hatua iliyotajwa kuwa inatishia utekelezaji wa mkataba wa amani.

Ni kwa kiasi gani mazungumzo haya yatakuwa na tija? Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa, akiwa Tanzania.

“Huenda kutapatikana suluhisho katika mkutano huo ama kutapatikana njia ambayo itawafanya wawili hao kuafikia makubaliano ambayo yatazuia nchi kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tena.” amesema Haji Kaburu.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani wa mwaka 2018, ambao haujatejelezwa kikamilifu, nafasi ya Waziri wa Ulinzi inapaswa kutolewa kutoka upanda wa Machar. 

Hata hivyo, Kiir amekiuka mkataba huo na kuamua kuwa Waziri ajaye wa Ulinzi atatoka kwenye chama chake huku ule wa usalama wa ndani atatoka upande wa Machar. 

Msemaji wa Puok Both Baluang, amesema mabadiliko hayo yanakwenda kinyume na mkataba wa amani, unaoweza kusababisha changamoto katika serikali ya pamoja kati ya Kiir na Machar katika siku zijazo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.