Pata taarifa kuu

Mali: Uongozi wa kijeshi umeahirisha kura ya maoni kuhusu Katiba mpya

NAIROBI – Uongozi wa kijeshi nchini Mali, umetangaza kuahirisha kura ya maoni kuhusu Katiba mpya, lakini umesisitiza kuwa, baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito, utaachia uongozi huo kwa raia.

Kiongozi wa kijeshi wa Mali  Assimi Goïta (Katikati)
Kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goïta (Katikati) © AP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa na msemaji wa serikali hiyo ya kijeshi Abdoulaye Maiga, ambaye amesema kura hiyo ya maoni iliyokuwa imeratibiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu wa Machi, imeahirishwa hadi tarehe nyingine.

Uongozi wa kijeshi chini ya Kanali Assimi Goita, ulikuwa umeahidi mabadiliko ya katiba kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Februari mwaka ujao.

Hata hivyo, uongozi huo unasema kura hiyo ya maoni haiwezi kufanyika kwa tarehe iliyotangazwa kwa sababu, inataka kuwaelimisha wananchi kuhusu rasimu hiyo ya katiba kabla ya kupangwa kwa tarehe nyingine, baada ya kushauriana pia na Tume ya Uchaguzi.

Tarehe 27 mwezi Februari, Kanali Goita aliyechukua madaraka ya nchi hiyo ya kijeshi,  alipokea rasimu ya katiba mpya na kuahidi nchi mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.