Pata taarifa kuu

Nigeria: Wavuvi 37 wamewauwa na watu wenye silaha Kaskazini Mashariki

NAIROBI – Wanajihadi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamewauwa wavuvi 37, katika eneo ambalo magaidi wa Boko Haram na wale wa Islamic State, wameendelea kuwalenga raia.

Wapiganaji wa Boko Haram na wale wa Islamic State wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia nchini Nigeria
Wapiganaji wa Boko Haram na wale wa Islamic State wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia nchini Nigeria AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yaliyotokea Jumatano ya wiki hii katika kijiji cha Guggo, umbali wa Kilomita 18 kutoka mji wa Dikwa, yanaaminiwa kutekelezwa na magaidi wa Boko Haram.

Miili ya wavuvi hao, ilipatikana mtoni na katika msitu ulio karibu na kijini hicho kwa mujibu wa Babakura Kolo kiongozi wa kundi la ulinzi la kijamii, linaloshirikiana na serikali.

Aidha, ameeleza kuwa kuna wasiwasi ya idadi ya vifo kuongzeka kwa sababu baadhi ya wavuvi walioshambuliwa wakati wakijiandaa na uvuvi, hawajapataikana.

Tangu mwaka 2009, kundi la Boko Haram limewauwa watu zaidi ya watu Elfu 40 na kusababisha wengine zaidi ya Milioni Mbili kuyakimbia makwao, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Mbali na Nigeria, Boko Haram inaendeleza shughuli zake nchini Niger, Chad na maeneo ya nchi ya Cameroon, inakoshirikiana na makundi mengine ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.