Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Barabara zilizo chini ya udhibiti wa M23 zafungwa

Makumi ya magari ya uchukuzi na abiria waliokuja kutoka kaskazini wamejikuta wamekwama na makabiliano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23. “Tulipofika Mweso tulikwama kwa sababu ya mapigano ya Kitshanga,” amesema dereva mmoja.

Waasi wa M23 karibu na eneo la Sake, magharibi mwa mji wa Goma, Novemba 30, 2012.
Waasi wa M23 karibu na eneo la Sake, magharibi mwa mji wa Goma, Novemba 30, 2012. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki kadhaa za vizuizi kwenye barabara, malori na abiria waliweza kuondoka katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kurejea katika mji wa Goma. Lakini barabara hizo zimefunguliwa kwa muda usiozidi saa 24, kulingana namashahidi waliohojiwa na shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa mko wa Kivu Kaskazini.

"Usafirishaji wa bidhaa na watu sasa umeidhinishwa" kwenye safu ya barabara zinazodhibitiwa na M23, Luteni Kanali Guillaume Ndjike, msemaji wa gavana wa mkoa huo alitangaza Jumatano jioni katika taarifa. Muda mfupi baada ya tangazo hili, msafara wa kwanza ulirudi Goma bila bila wasiwasi wowote.

Hatua hiyo "imesitishwa hadi itakapotangazwa tena", gavana huyo amesema siku ya Alhamisi leo mchana katika taarifa yake mpya, akisema waasi "wamemuua dereva mmoja" na "kupora bidhaa zote". Tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022, M23 imechukua sehemu kubwa za mkoa wa Kivu Kaskazini, na hivyo kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara kuu za mkoa huo.

"Nimefika (Goma) baada ya mateso makubwa. Tulikaa huko kwa miezi miwili, tulilala chini ya magari," Zawadi Kavira, abiria aliyekwama Mweso, ameliambia shirika la habri la AFP siku ya Alhamisi, kilomita 100 kaskazini mwa Goma.

Mji huu wenye wakazi wapatao 60,000 ulikuwa chini ya udhibiti wa waasi tarehe 26 Januari. Tangu wakati huo, M23 wamepiga hatua na wanaendelea kusonga mbele kuelekea Goma, jiji lenye wakazi zaidi ya milioni moja, linalopakana na mpaka wa Rwanda upande wa mashariki, Ziwa Kivu upande wa kusini na waasi kaskazini na magharibi.

Mnamo Februari 28, kundi la wabunge kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini na uwakilishi wa mkoa wa shirikisho la kampuni za congo (FEC), katika barua mbili tofauti, walimuomba gavana na rais wa Jamhuri kufungua tena barabara ili "kuruhusu usafirishaji wa vyakula katika jiji la Goma", ilibainisha FEC.

Gavana huyo alijibu vyema ombi lao "kwa maslahi ya raia wanaokabiliwa na athari za vita", kabla ya kutafakari upya uamuzi wake siku iliyofuata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.