Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi aishutumu Rwanda kwa kuchochea machafuko eneo la Mashariki

NAIROBI – Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, ameendelea kuinyooshea kidole nchi ya Rwanda, kwa kile anachodai inachochea machafuko mashariki mwa nchi hiyo, akikanusha nchi yake kuwashambulia raia wake wanaozungumza Kinyarwanda.

Félix Tshisekedi, Rais wa DRC
Félix Tshisekedi, Rais wa DRC AP - Tobias Schwarz
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ametoa matamshi haya akiwa ziarani mjini Geneva, Uswis, ambapo amesisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa raia wa nchi hiyo katika kukabiliana na makundi ya waasi.

“Viongozi wa Rwanda wamefufua kundi la M23 ilikuivamia DRC na kuzuia mchakato wa utekelezwaji wa amani wa Nairobi ilikuendeleza wizi wa rasilimali ya DRC.”amesema rais Felix Tshisekedi.

Kigali kwa upande wake imeendelea kukanusha tuhuma za DRC kuwa inawaunga mkono waasi wa M23 wanaoendelea kuwashambulia raia katika maeneo ya mashariki ya Congo.

Licha ya waasi hao kutakiwa kuondoka katika maeneo wanayoshikilia nchini DRC, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.