Pata taarifa kuu

Kenya: Jill Biden ahimiza wanawake kuungana pamoja ili kujiendeleza

Jill Biden, mke wa rais wa Marekani, ameendelea na ziara yake nchini Kenya, kwa kukutana na makundi ya wanawake na kuwahimiza kuunganisha nguvu kwa ajili ya maendeleo yao. 

Mkewe rais wa Marekani, Jill Biden.
Mkewe rais wa Marekani, Jill Biden. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na viongozi wanawake katika makazi ya balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman, Ijumaa jioni muda mfupi tu baada ya kuwasili nchini humo, Dr. Biden amesisitiza umuhimu wa kimkakati wa Kenya kwa Marekani.

Wanawake wanapopata hela, wanawekeza katika familia, hilo ni hakika kwa sababu mimi ni mfanyakazi  na tunageuka kuwa walimu na kuwasaidia watu wengine kupata wanachokitaka. Tuna uwezo wa kuunda nafasi za ajira na wanawake wanapopata fursa ya kushiriki katika masuala muhimu katika jamii, tunasaidia kuleta uthabiti na utulivu. 

Siku ya Jumamosi, Dr. Biden alizuru mradi wa benki ya mezani katika eneo bunge la Kibera, katika kaunti ya Nairobi, mradi unaoongozwa na Mke wa Rais wa Kenya Rachel Ruto.

Jill Biden aliwasili nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu, baada ya kutokea Namibia kwa ziara ya siku mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.