Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mia moja wauawa ndani ya wiki mbili katika mapigano Somaliland

Takriban watu 96 wamefariki katika mji wa Somaliland, eneo linalozozaniwa nchini Somalia ambako mapigano yamezuka kwa muda wa wiki mbili kati ya wanamgambo watiifu kwa serikali ya Somalia na vikosi vinavyotaka kujitenga, mkurugenzi wa hospitali kuu ya eneo hilo amesema leo Alhamisi.

Kiongozi muhimu wa kitamaduni wa Somaliland, aliyehusika katika mapigano dhidi ya wanajeshi wa vikosi vilivyojitenga, kwa upande wake aliwaambia waandishi wa habari huko Las Anod siku ya Jumatano jioni kwamba zaidi ya watu 150 waliuawa.
Kiongozi muhimu wa kitamaduni wa Somaliland, aliyehusika katika mapigano dhidi ya wanajeshi wa vikosi vilivyojitenga, kwa upande wake aliwaambia waandishi wa habari huko Las Anod siku ya Jumatano jioni kwamba zaidi ya watu 150 waliuawa. © RFI
Matangazo ya kibiashara

"Tuna maiti 96 na majeruhi 560 wameorodheshwa katika hospitali kuu" katika mji wa Las Anod, Ahmed Mohamed Hassan ameliambia shirika la habri la AFP kwa njia ya simu.

Kiongozi muhimu wa kitamaduni wa Somaliland, aliyehusika katika mapigano dhidi ya wanajeshi wa vikosi vilivyojitenga, kwa upande wake aliwaambia waandishi wa habari huko Las Anod siku ya Jumatano jioni kwamba zaidi ya watu 150 waliuawa. "Idadi ya vifo ilifikia watu 150 na wengine zaidi ya 500 walijeruhiwa," alisema afisa huyo, Garaad Jama Garaad Ali.

Eneo la zamani la Uingereza, Somaliland lilijitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991, kitendo ambacho hakijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Vurugu za hivi punde zaidi huko Las Anod zilianza siku 17 zilizopita, Februari 6, saa chache baada ya machifu wa kimila kutoa taarifa ya kuahidi kuunga mkono "umoja na uadilifu wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia", na kuzitaka mamlaka za Somaliland kuondoa vikosi vyao kutoka eneo hilo.

Usitishaji mapigano ulitolewa mnamo Februari 10 na mamlaka, lakini pande hizo mbili zinashutumiana kila upande kwa kukiuka makubaliano ya usitihwaji mapigano. Hasa, mapigano hayo yameripotiwa tena Alhamisi, kulingana na mashahidi na machifu wa kimila.

"Mapigano yalianza mapema asubuhi na tayari mabomu kadhaa yameanguka kwenye mji," Mohamed Saleban, ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu, akisema watu wametoroka makazi yao.

Mnamo Februari 16, Ofisi ya ndani ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (Ocha) ilitangaza kuwa zaidi ya watu 185,000, 89% yao wakiwa wanawake na watoto, wamekimbia ghasia huko Las Anod.

Somaliland, eneo lenye watu milioni 4.5, limesalia kuwa maskini na limetengwa lakini lina utulivu kiasi kwani Somalia imeharibiwa na miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na uasi wa Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.