Pata taarifa kuu

Burkina Faso yajiandaa kwa maziko ya mabaki ya Thomas Sankara na wenzake

Sherehe hiyo itafanyika katika eneo la ukumbusho wa Thomas Sankara, ambapo aliuawa mwaka wa 1987. Sherehe kuu ya baba wa mapinduzi itafanyika mnamo Oktoba 15. Familia yake haitashiriki katika mazishi haya kwa sababu walitaka mwili wake uhifadhiwe kwenye eneo lingine.

Lango la makumbusho ya Thomas Sankara katika eneo la Baraza la Makubaliano, Ougadougou, Machi 3, 2019.
Lango la makumbusho ya Thomas Sankara katika eneo la Baraza la Makubaliano, Ougadougou, Machi 3, 2019. © Creative Commons
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kukataa kwa familia yake, mabaki ya Thomas Sankara yatazikwa tena kwenye eneo la Baraza la makubaliano. Uchaguzi wa mahali hapa unasimamiwa na "masharti ya kijamii-utamaduni na usalama wa maslahi ya taifa", kulingana na serikali, ambayo inabainisha kuwa sherehe za mazishi zitafanyika kulingana na taratibu za kitamaduni na za kidini.

Tayari makaburi yamejengwa.

"Familia yetu bado iko kwenye mtihani mzito, amesema Blandine Sankara, dada mdogo wa rais wa zamani na msemaji wa familia, kuona Thomas Sankara akizikwa kinyume na matakwa yetu, mahali ambapo aliuawa. "

Watoto wa mwanahabari Paulin Bamouni pia hawatakuwepo. Ikiwa walipata haki ya kuleta jeneza kwa ajili ya mabaki ya baba yao, wkwa kushindwa kumzika tena wao wenyewe, wanabaini kwamba "imani zao za kibinafsi [...] haziruhusu kushiriki katika sherehe": " Miaka 35 baadaye, historia inaonekana kujirudia! Anauawa mara ya pili mbele ya macho yetu, ” Céline Bamouni, bintiye mshauri wa zamani wa Thomas Sankara anaelezea masikitiko yake.

Ni hali ya kusikitisha kulingana na Profesa Albert Ouedraogo, profesa wa fasihi simulizi ya Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Joseph Ki Zerbo, ambaye anabaini kwamba mazishi ni wakati ambapo walio hai na wafu huwa sehemu moja

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.