Pata taarifa kuu

DRC: Mapigano kati ya FARDC na M23 yazua hofu mjini Sake

NAIROBI – Mashariki mwa DRC kumeripotiwa kuendelea kwa mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali FARDC na waasi wa M23, kilomita chache magharibi mwa mji wa Sake, jimboni Kivu Kaskazini.

Wakaazi wa Sake wakikimbia mapigano kati ya M 23 na wanajeshi wa FARDC
Wakaazi wa Sake wakikimbia mapigano kati ya M 23 na wanajeshi wa FARDC © Benjamin Kasembe
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Sake ni eneo la kimkakati linalounganisha na mji wa Goma kilomita 30.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, mapigani yalianza Jumatano asubuhi kuelekea mchana, ambapo waasi wa M23 walioko kwenye milima ya Kagoma ambako kuna kambi ya jeshi la Serikali walishambulia.

Mvua kubwa na hali mbaya ya hewa haikuwawezesha wanajeshi wa Serikali kusaidiwa kwa mashambulio ya anga ili kuwadhibiti waasi hao.

Milio ya risasi na milipuko ilisikika kwenye mji wa Sake ambao tangu Februari 9 umekuwa ukilengwa na waasi hao lakini wanajeshi wa Serikali walifanikiwa kuzima jaribio lao.

Jumatano hii raia walionekana kupatwa na sintofahamu wengi wakikimbia kuelekea mji wa Goma, kama anavyoeleza mmoja wa raia hao.

"Tulitoroka mapigano kwa sasa hatujui ni wapi tunaelekwa wapi."ameeleza raia wa Goma.

Mji wa sake ni êneo lenye wanajeshi wa Monusco kutoka mataifa kadhaa ikiwemo tanzania, malawi, Guatamala, India na Afrika Kusini, na kwamujibu wa vyanzo vyetu, wanajeshi hawa bado wapo kwenye kambi zao.

Ikiwa waasi watafanikiwa kudhibiti njia za kuelekea Mushaki, kilomita 7 na mji wa Sake, huenda kukatatiza kampeni ya utoaji misaada jimboni Kivu Kaskazini, unaopakana na Goma na mpaka wa Rwanda, êneo hili likitatuizika mara kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.