Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Burkina Faso: Takriban wanajeshi 51 wauawa katika shambulizi la kuvizia

Nchini Burkina Faso, wanajeshi wasiopungua 51 waliuawa katika shambulio la siku ya Ijumaa, Februari 17, katika eneo la Sahel, kulingana na ripoti ya awali kutoka makao makuu ya jeshi. Mapigano makali yaliripotiwa kati ya wanajeshi wa Burkina Faso na kundi la kigaidi leye silaha kati ya maeneo ya Oursi na Deou, katika jimbo la Oudalan.

Shambulio hilo lilitokea kati ya maeneo ya Oursi na Deou, katika ejimbo la Sahel, karibu na mpaka na Mali.
Shambulio hilo lilitokea kati ya maeneo ya Oursi na Deou, katika ejimbo la Sahel, karibu na mpaka na Mali. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Idadi hii inaweza kuongezeka katika saa zijazo kwa sababu wanajeshi kadhaa bado hawajulikani walipo. "Karibu watu 80 bado wanatafutwa," chanzo cha usalama kimeiambia RFI, saa chache kabla ya kutangazwa kwa idadi hii ya vifo vya wanajeshi 51 upande wa jeshi la Burkina Faso.

Waliojeruhiwa wanatibiwa katika vituo vinavyofaa vya matibabu kwa ajili ya huduma, na helikopta za jeshi la anga zimeanza kusafirisha miili ya wanajeshi waliouawa wakati wa shambulio hili kwenda mji mkuu Ouagadougou.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa majeshi, wanajeshi wa Burkina Faso walikuwa katika kazi yao ya kila siku waliposhambuliwa na watu wenye silaha. "Kikosi hicho kililengwa na shambulio tata," mamlaka imesema, na "mapigano makali yakatokea. "

Shambulio hilo lilifanyika kati ya maeneo ya Oursi na Deou, katika eneo la Sahel, karibu na mpaka na Mali. Wanajeshi wengi walitumwa kwenye eneo la tukio wikendi nzima.

Kulingan na duru za kijeshi magaidi zaidi ya mia moja waliuawa na magari kadhaa pamoja na vifaa vya kijeshi kuharibiwa. Washambuliaji walikuwa wakijaribu kutoroka kuvuka mpaka wa kaskazini kuelekea Mali, wakati walilengwa na jeshi la anga la Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.