Pata taarifa kuu

Niger: Watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi la 2021 wakabiliwa na adhabu kali

Kutoka miaka miwili hadi thelathini ya kifungo kigumu, hizi ndizo hukumu zilizoombwa na mwendesha mashitaka wa serikali ya Niger katika kesi ya jaribio la mapinduzi, saa 48 kabla ya kuapishwa kwa rais mpya mteule Mohamed Bazoum, katika matokeo ya kesi ambayo mawakili wa washtakiwa wamekana kila kitu. Mawakili waliofikia hatua ya kutaja jaribio la mapinduzi kama "mchezo wa andani" ulioandaliwa na mamlaka iliyopo.

Kesi hiyo, ambayo ilifanyika ndani ya uwanja wa kambi ya askari, imedumu siku ishirini na nane.
Kesi hiyo, ambayo ilifanyika ndani ya uwanja wa kambi ya askari, imedumu siku ishirini na nane. AP - Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo, iliyofanyika ndani ya uwanja wa kambi ya askari- iliyodumu kwa siku ishirini na nane - iliwezesha pande zote zinazohusika, washtakiwa 58 na mawakili hasa, kutoa mwanga kwa raia, ambao walikuja kwa wingi, kuhusiana na jaribio la mapinduzi ambalo karibu, usiku wa Machi 30 hadi 31, 2021, lilipindua utawala wa Rais wa zamani Issoufou Mahamadou.

Katika shtaka lake, mwendesha mashitaka huyo wa serikali amewashambulia kwa nguvu zote watu hao wanaodaiwa kuwa waasi, na kuwaita kundi la maafisa wasiojua hatari kubwa inayotishia nchi kwa kula njama dhidi ya serikali. Jenerali Abou Tarka amekwenda mbali zaidi, akisisitiza kwamba waliwasaliti watu kwa kubadilisha silaha zilizopatikana kwa ushuru wa wananchi wa Niger dhidi ya viongozi waliochaguliwa. Wamevuka livuka mstari mwekundu, Naibu mwendesha mashitaka wa serikali amesema.

Adhabu zinazohitajika ni kati ya miaka miwili hadi thelathini gerezani kwa maafisa waliohitimu kama waanzilishi wa jaribio hilo. Matoleo pia yaliombwa kwa ushahidi wa kutosha. Kwa muda wa saa 48, mawakili hao, ishirini kwa idadi, walijaribu kusambaratisha kile walichokiita "kizushi" kilichoandaliwa na Niamey ili kuwazuia askari wasumbufu; mwenyekiti Yaye Mounkaila atasema kuwa wanaoonyeshwa kuwa wahusika wakuu wamerubuniwa kuwafikia wenzao wakiwa wamebeba silaha.

Hukumu itatolewa tarehe 24 Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.