Pata taarifa kuu
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Tunisia: Waandishi wa habari walaani 'vitisho' kutoka mamlaka

Makumi ya waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu wameandamana siku ya Alhamisi mjini Tunis kupinga sera wanayoitaja kuwa ya ukandamizaji kutoka mamlaka inayolenga kuvitisha vyombo vya habari.

Wanahabari wa Tunisia wakati wa maandamano ya uhuru zaidi wa vyombo vya habari, mbele ya makao makuu ya chama cha Wanahabari wa Tunisia (SNTJ) mjini Tunis, Mei 5, 2022.
Wanahabari wa Tunisia wakati wa maandamano ya uhuru zaidi wa vyombo vya habari, mbele ya makao makuu ya chama cha Wanahabari wa Tunisia (SNTJ) mjini Tunis, Mei 5, 2022. © AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

"Hapana kwa ukandamizaji wa waandishi wa habari", "Tunadai vyombo vya habari kuwa huru na kujitzgzmea", "Aibu kwa ikulu ya rais ambayo inataka kuzuia uhuru wa waandishi wa habari", wamekuwa wakiimba waandamanaji waliokusanyika karibu na ofisi ya rais huko Tunis, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Baadhi ya waandamanaji walivaa kanda nyekundu midomoni mwao wakiashiria nia ya mamlaka ya kuvifunga vyombo vya habari. Wawakilishi wa mashirika ya kiraia na wanaharakati kutoka shirika linalotetea Haki za Kibinadamu la Tunisia walishiriki katika maandamano haya kwa wito wa chama cha Wanahabari wa Tunisia (SNJT).

Kikosi kikubwa cha polisi kilitumwa kuwasimamia waandamanaji na kuwazuia kukaribiamakao makuu ya serikali. "Mamlaka inataka kuvinyamanzisha vyombo vya habari vya kibinafsi na vya umma na kukamatwa kwa mkurugenzi wa (kituo cha redio cha kibinafsi) Mosaïque FM ni jaribio la kuitisha sekta hii," amesema Mahdi Jlassi, kiongozi wa SNJT.

Watu kumi walikamatwa kati ya Jumamosi na Jumatatu, akiwemo Noureddine Boutar, mmiliki wa Mosaïque FM, maarufu sana nchini Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.