Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DR Congo yazungumzia mpango wa jeshi la EAC kuhusu M23

NAIROBI – Baada ya wakuu wa Majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana jijini Nairobi wiki iliyopita, na kutangaza makataa mapya kwa waasi wa M 23 kujiondoa katika maeneo wanayoshikilia jimboni Kivu Kaskazini, kuanzia tarehe 28 mwezi huu kwa kipindi cha siku thelathini, serikali jijini Kinshasa, imezungumzia hatua hiyo.

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na waasi mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa EAC wanaopambana na waasi mashariki mwa DRC AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Christophe Lutundula Waziri wa Mambo ya nje wa DRC amesema

“Ratiba ya Luanda haikuheshimiwa na sasa kuna ratiba nyengine tuko makini zaidi tutafuatilia sana, kikosi cha kikanda hakijaridhisha matarajio yetu.” ameeleza Christophe Lutundula.

Raia katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiaandamana kwa kile wanachodai ni kutoridhishwa na utendakazi wa vikosi vya jumuiya ya Afrika mashariki.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.