Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Côte d'Ivoire: Ndugu wawili wa Guillaume Soro waachiliwa baada ya kukata rufaa

Ndugu wawili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire Guillaume Soro wameachiliwa huru Jumatatu na Mahakama ya Rufaa ya Abidjan, ambayo pia imethibitisha kuhukumiwa kwa washtakiwa wengine kadhaa kwa 'jaribio la kuhatarisha usalama wa taifa.'

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imethibitisha kwamba bado inachunguza uhalifu unaoweza kuwa ulifanywa na kambi ya Alassane Ouattara, inayoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Guillaume Soro. Hapa, kabla ya mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Septemba 17, 2020.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imethibitisha kwamba bado inachunguza uhalifu unaoweza kuwa ulifanywa na kambi ya Alassane Ouattara, inayoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Guillaume Soro. Hapa, kabla ya mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Septemba 17, 2020. © Stéphane de Sakutin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa zamani wa Bw. Soro, Félicien Sékongo, na waziri wa zamani Alain Lobognon, waliohukumiwa Juni 2021 hadi miezi 17 jela, wameachiliwa huru Jumatatu. Washtakiwa wengine tisa, akiwemo Souleymane Kamagaté, almaarufu "Soul to Soul", mkuu wa zamani wa itifaki ya Bw. Soro, walihukumiwa, kama ilivyokuwa mwanzo, kifungo cha miaka 20 jela.

"Haki pekee tuiyo nayo ni ile ya kukata rufaa katika kesi, na tutafanya hivyo", ametangaza mmoja wa mawakili wa utetezi, bwana Raoul Gohi Bi. "Ni hisia ya kukata tamaa kabisa," ameongeza.

Kaka zake Guillaume Soro, Rigobert na Simon, waliohukumiwa mwaka wa 2021 hadi miezi 17 jela kwa "kuvuruga usalama wa umma", hawakuwapo mbele ya Mahakama ya Rufaa. Hukumu yao pia imethibitishwa.

Guillaume Soro, 50, mshirika wa zamani wa Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, anatuhumiwa kuanzisha "uasi wa kiraia na kijeshi" na wafuasi wake wakati aliporejea nchini mwake mnamo mwezi Desemba 2019.

Akiwa uhamishoni katika eneo lisilojulikana tangu 2019, baada ya kuzorota kwa kasi kwa uhusiano wake na Bw. Ouattara, Spika wa zamani wa Bunge la Kitaifa alihukumiwa kifungo cha maisha bila kuwepo mwaka wa 2021. Rufaa yake ilionekana kuwa isiyokubalika.

Kiongozi wa uasi uliotawala nusu ya kaskazini ya Côte d'Ivoire katika miaka ya 2000, Guillaume Soro alimsaidia Alassane Ouattara kuingia madarakani wakati wa mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011 ambao ulitokea baada ya kukataa kwa Rais Laurent Gbagbo kukubali kushindwa katika uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwaka 2010.

Guillaume Soro alikuwa kiongozi wa kwanza wa serikali ya Bw. Ouattara, kabla ya kuhitilafiana mapema 2019, kutokana na, kulingana na waangalizi, na nia ya Bw. Soro kuwania katika uchaguzi wa urais.

Mnamo Aprili 2020, Bw. Soro alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kashfa ya ubadhirifu wa fedha za umma kwa kujaribu, kulingana na mahakama, kuidhinisha nyumba iliyonunuliwa na Serikali ili kumhifadhi alipokuwa Waziri Mkuu. Hukumu hii ilihalalisha kubatilisha ugombea wake katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.