Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Gabon: hakuna waangalizi wa EU katika uchaguzi ujao

Nchini Gabon, hakutakuwa na waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) katika uchaguzi ujao. Gabon itafanya chaguzi tatu mwaka huu, uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu uchaguzi wa rais, wabunge na serikali za mitaa. Lakini maafisa wa EU walitangaza kuwa hawatatuma timu za kufuatilia mchakato wa upigaji kura. Hii ikiwa ni ishara ya wasiwasi kwa upinzani.

Libreville, mji mkuu wa Gabon.
Libreville, mji mkuu wa Gabon. Getty Images/Gallo Images ROOTS Collection - Robert Ross
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa mpinzani Jean-Gaspard Ntoutoume Ayi, anasema kukosekana kwa waangalizi hawa kunaonyesha kuwa halisio nzuri: "Ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Ulaya unajulikana kama dhamira ya uchunguzi wa kina na wa kuaminika. Ukweli kwamba hawajaalikwa na serikali ya Gabon unaonyesha jinsi serikali ya Gabon inavyotarajia kuona uchaguzi ujao ukifanyika. Serikali ambayo ina nia ya kulazimisha kupitisha na kuvuruga uchaguzi haina nia ya kuleta ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya.

Mvutano

Pierre-Claver Maganga Moussavou ni kiongozi wa Social Democratic Party (PSD). Anaomba Umoja wa Ulaya kwenda kwenye kutokubali uchaguzi kufanyika bila wao kuhudhuria: "Ninafikiria juu ya kutotoa msaada kwa mtu yeyote aliye hatarini. Umoja wa Ulaya hauwezi kukata tamaa. Umoja wa Ulaya unaweza kulazimisha waangalizi wake kwa sababu kuna kuingiliwa kulazimisha demokrasia. Inatosha tu uchimbaji wa mafuta ukome na mkiacha  kutumia mafuta hayo, Gabon haina rasilimali zaidi”.

Chanzo kilicho karibu na utawala wa Gabon kinabaini kuwa mzozo wa kidiplomasia wa 2016 umeacha makovu yake hata leo. Kwa vyovyote vile, wapinzani wanaamini kwamba hakuna shirika lingine la kimataifa linaloweza kutuma ujumbe wa uchunguzi unaoaminika kama ule wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.