ETHIOPIA: Raia washiriki kura ya maamuzi ili kuundwa kwa jimbo jipya
Raia wa Ethiopia, Kusini mwa nchi hiyo, wamepiga kura kuamua iwapo nchi hiyo iwe na jimbo la 12.
Imechapishwa:
Cheza - 00:40
Zaidi ya wapiga kura Milioni tatu wameshiriki katika zoezi hilo, na matokeo yanatarajiwa tarehe 15 mwezi huu.
Lakini je ni kwa nini Ethiopia imeendelea kukumbatia uongozi wa majimbo? Lee Ndlela, mchambuzi wa siasa za Kimataifa, anaeleza akiwa jijini Nairobi.
“Inaweza fanya watu waungane pamoja, tena inaweza fanya watu wasikuwe na amani nchini humo.” amesema Lee Ndlela
Waziri Mkuu Abiy Ahmed tangu alipoingia madarakani mwaka 2018, ameongoza kuundwa kwa majimbo mengine mawili ya Sidama mwaka 2019 na Kusini Magharibi 2021.