Pata taarifa kuu
DRC-MISAADA YA KIBINADMU

DRC: Zaidi ya watu millioni 26 watahitaji misaada ya kibinadamu:OCHA

Ofisi ya umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, imesema watu zaidi ya milioni 26 watahitaji msaada wa kibinadamu nchini DRC.

Raia wanaotoroka makwao kwa hofu ya kushambuliwa na waasi wa M23 mashariki mwa DRC
Raia wanaotoroka makwao kwa hofu ya kushambuliwa na waasi wa M23 mashariki mwa DRC © ALEXIS HUGUET/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa OCHA, mwaka wa 2022 ulikumbwa na michakato kadhaa ya kisiasa katika muktadha wa kikanda na kitaifa ulioshuhudia uwepo na shughuli za makundi kadhaa yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo na hasa kuzuka tena kwa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini. 

Aidha, kuendelea kwa mizozo ya makundi yenye silaha na kijamii jamii kumesababisha idadi kubwa ya watu kufariki katika eneo la Mashariki. 

OCHA inasema kati ya zaidi ya watu milioni 5.7 waliolazimika kuhama makazi yao nchini DRC, zaidi ya asilimia 80 walifanya hivyo kutokana na mashambulio ya makundi yenye silaha, ambayo kwa asilimia 97 yametokea mashariki mwa nchi hiyo, watu takriban milioni mbili wakikimbia makwao tangu mwezi januari. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.