Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI: ZIARA YA PAPA FRANCIS

Papa Francis ahitimisha ziara Sudan Kusini akihimiza amani na utangamano

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, amehitimisha rasmi ziara yake nchini Sudan Kusini, ambapo amezitaka pande zinazozozana kuweka chini kile alichosema “silaha za chuki”.

Papa Francis amehitimisha ziara yake barani Afrika
Papa Francis amehitimisha ziara yake barani Afrika AFP - TIZIANA FABI
Matangazo ya kibiashara

Licha ya mkataba wa amani uliotiwa saini na rais Salva Kiir na hasimu Wake Riek Machar, bado machafuko yameendelea kushuhudiwa nchini humo, rais Kiir akiahidi kufufua tena mazungumzo yaliyokuwa yanaratibiwa na ofisi ya Papa mjini Rome.

Katika kuheshimu ziara ya Papa Francis, na ikizingatiwa huu ni mwaka wa amani na maridhiano, natangaza rasmi kuanza kwa mazungumzo ya amani mjini Roma.” amesema Salva Kiir.

Rais Kiir ametoa tangazo hili akiurai upinzani pia kujiunga katika mazungumzo haya ili kuwepo mwafaka wa kudumu na kumaliza mgogoro wa tangu mwaka 2011.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.