Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Burkina Faso: Takriban watu ishirini a nane wauawa katika mashambulizi Cascades na Sahel

Nchini Burkina Faso, takriban watu 28 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti. Shambulio la kwanza limetokea katika eneo la Cascades magharibi mwa nchi hiyo ambalo lmegharimu maisha ya watu  15. Na shambulio la pili, limetokea huko Falangoutou katika eneo la Sahel ambalo limeua watu 13, wakiwemo askari 10.

Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya NAABA Koom, Septemba 29, 2015.
Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya NAABA Koom, Septemba 29, 2015. REUTERS/Arnaud Brunet
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo mawili yalitokea Siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi iliyotolewa Jumanne. Taarifa hii inasema "shambulio la kigaidi" dhidi ya askari na wanajeshi wa kujitolea kwa ulinzi wa chi, wasaidizi wa jeshi la Burkina Faso, waliokuwa wakipiga kambi huko Falagountou, eneo ambalo liko mbali na mpaka na Niger.

Makao makuu ya jeshi yanasema wahusika wa shambulio hilo ni "kundi lenye silaha" ambalo "lilijitolea kushambulia raia" baada ya "kushindwa wiki chache zilizopita na vikosi vilivyojitolea kurejesha maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya wapiganaji ". Jeshi linabainisha kuwa "takriban miili kumi na tano ya magaidi ilipatikana wakati wa shughuli za jeshi. "

Mwezi mbaya wa Januari

Alhamisi, Januari 25, takriban raia kumi na wawili waliuawa katika mashambulizi mawili huko Dassa, katikati-magharibi mwa Burkina Faso, takriban kilomita 140 kutoka Ouagadougou. Wiki moja kabla, eeo la kaskazini mwa nchi lilikumbwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya. Makao makuu ya jeshi yametoa wito kwa raia kuwa "wasikatishwe tamaa na adui na kuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa vikosi vya jeshi na usalama vikisaidiwa na wanamgambo wanaojitolea

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.