Pata taarifa kuu
DRC- RWANDA- USALAMA

Rwanda yaituhumu DRC kwa kukiuka anga yake, Kinshasa yakanusha

Saa chache baada ya utawala wa Rwanda kudai umechukua hatua kwa ndege ya kivita ya DRC baada ya kuingia kwenye anga yake, Serikali ya Kinshasa, imekanusha madai hayo, ikisisitiza ndege yake ilikuwa katika ardhi yake.

Rais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC , Marchi 2021
Rais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC , Marchi 2021 © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na msemaji wa Serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, jeshi la nchi hiyo lilifyatua risasi za onyo kwa ndege ya DRC aina ya Sukoi 25, aliyodai ilivuka mpaka na kuingia kwenye êneo la anga ya mji wa Rubavu jirani na Goma.

Taarifa ya Rwanda imeongeza kuwa, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa ndege ya kivita ya DRC kutumia anga lake vibaya, ambapo mara ya mwisho hata waliiruhusu kutua kabla ya kurejea Congo.

Hata hivyo utawala wa Kinshasa kupitia wizara ya mawasiliano, imekanusha ndege yake kutumia anga ya Rwanda, msemaji wa Serikali ¨Patrick Muyaya, akisema ndege yao ilishambuliwa ikiwa ndani ya ardhi yake.

Aidha tarifa ya Serikali ya DRC, bila ya kuweka wazi hatua ambazo itachukua, ilisema haitafumbia macho kitendo kilichofanywa na Rwanda, na kwamba kama nchi inayo haki ya kujilinda na kulinda mipaka yake, ikitaja kitendo hiki kama kuanzisha vita.

¨Picha za vídeo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zimeonesha mlipuko wa kile kinachodhaniwa roketi, nyuma ya mkia wa ndege hiyo ambayo baadae ilifanikiwa kutua salama katika uwanja wa kimataifa wa Goma.

Tukio hili linajiri wakati ambapo uhusiano baina ya nchi hizo mbili jirani, unaendelea kuzorota, Kinshasa ikiutuhumu utawala wa Kigali kwa kuwasaidia waasi wa M23, Rwanda ikikanusha tuhuma hizo ambazo hata wataalamu wa umoja wa Mataifa wamethibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.