Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

Abdirizaki Mukhtar Garad anayetuhumiwa kushambulia kanisa DRC ni nani?

Msikilizaji mamlaka nchini Kenya, zinaendelea na uchunguzi kubaini namna raia wake aliyekamatwa nchini DRC akituhumiwa kuhusika na shambulio bomu kwenye kanisa la Kasindi, mashariki mwa nchi hiyo, aliweza kusafiri.Hii sio mara ya kwanza kwa raia wa Kenya kutuhumiwa kufanya ugaidi nchini DRC, je tunafahamu nini kuhusu mtuhumiwa huyu ?Mwandishi wetu Emmanuel Makundi, ana maelezo zaidi…

Wanajeshi wa FARDC wakiwapa ulinzi raia katika eneo la Bunia DRC
Wanajeshi wa FARDC wakiwapa ulinzi raia katika eneo la Bunia DRC © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kitengo cha polisi wa kupambana na ugaidi nchini Kenya, mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka eneo la Wajiri, alikamatwa siku ya Jumapili na ametambuliwa kuwa ni Abdirizaki Mukhtar Garad.

Licha ya kutotoa taarifa zaidi kumuhusu, idara za usalama zinaendelea na uchunguzi, ikiwa ni mwaka mmoja pia umepita tangu raia wake mwingine Rashid Mohamed, akamatwe akihusishwa kushirikiana na kundi la ADF akiwa amepigana kwenye nchi za Somalia na Msumbiji.

Kwa miaka kadhaa sasa kundi la ADF lenye uhusiano na Islamic State, limekuwa likipanua wigo wa kusajili wapiganaji kutoka kwenye nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Uganda, Kenya na Tanzania.

Mwaka 2021, serikali ya Marekani ilitangaza kuwawekea vikwazo raia kadhaa wa Kenya, wanaotuhumiwa kutoa ufadhili kwa kundi la ADF na Islamic State ambalo limekiri kuhusika na shambulio la Jumapili nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.