Pata taarifa kuu

Jeshi la Somalia laichukua tena bandari iliyokuwa ikishikiliwa na Al-Shabab kwa miaka 10

Jeshi la Somalia limepata tena udhibiti wa bandari "ya kimkakati" waliyoikalia kwa zaidi ya muongo mmoja kutoka kwa Waislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab, Waziri Mkuu na vyanzo vya usalama wametangaza siku ya Jumatatu.

Jeshi la Marekani lilisema kuwa liliendesha mashambulizi dhidi ya Al Shabab katika eneo la Harardhere kilomita zaidi ya mia moja kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu Oktoba 12, 2018.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa liliendesha mashambulizi dhidi ya Al Shabab katika eneo la Harardhere kilomita zaidi ya mia moja kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu Oktoba 12, 2018. GOOGLE MAPS
Matangazo ya kibiashara

Harardhere, mji wa bandari ulioko takriban kilomita 500 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, ulikuwa umedhibitiwa tangu mwaka 2010 na kundi la Al Shabab, linaloshirikiana na Al-Qaeda. "Ni ushindi wa kihistoria, wanajeshi jasiri wa jeshi la taifa (wameukomboa mji wa kimkakati wa bandari wa Harardhere," Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre amesema siku ya Jumatatu.

"Taarifa tulizokuwa nazo zinaonyesha kuwa magaidi (Al Shabab) walikuwa wakitumia mji wa pwani kupata vifaa," Hussein Ahmed, Waziri wa posta, ameliambia shirika la habari la AFP.

Waziri huyo, pamoja na vyanzo vya usalama, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba jiji hilo limechukuliwa tena bila mapigano yoyote, Al Shabab wamejiondoa kabla ya kuwasili kwa vikosi vya serikali.

Al Shabab wamekuwa wakipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu 2007. Al Shabab ambao wamefukuzwa nje ya miji mikuu ya nchi mwaka 2011-2012, wamesalia kuwa imara katika maeneo makubwa ya vijijini.

Serikali ya Hassan Sheikh Mohamoud imeahidi "vita vya kila namna" dhidi ya kundi hili la Kiislamu, ambapoo wapiganaji wakeBw Mohamoud hivi majuzi aliwaita "kunguni". Mnamo mwezi Septemba, alituma jeshi, ikiwa ni pamoja na vikosi maalum, kusaidia wanamgambo wa ndani, wanaojulikana kama "Macawisley", ambao waliasi dhidi ya Al Shabab.

Mashambulizi haya, yakiungwa mkono na jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) na mashambulizi ya anga ya Marekani, yalifanya iwezekane kuteka tena maeneo makubwa katika majimbo mawili katikati mwa nchi, Hirshabelle ambako kunapatikana mkoa wa Hiran na Galmudug.

Lakini Al Shabab wanaendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kulipiza kisasi. Watu 19 waliuawa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari huko Mahas, mji wa Hiran, mapema mwezi huu.

Tarehe 29 Oktoba, magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu yalilipuka ndani ya dakika chache katika mji mkuu Mogadishu, na kuua watu 121 na wengine 333 kujeruhiwa, katika shambulio baya zaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika kipindi cha miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.